FOLLOWERS

Friday, October 28, 2011

SIMBA VS YANGA, KIVUMBI KESHO

 Wachezaji wa timu ya Simba wakiomba dua katika moja ya mechi za na watani wao wa jadi Yanga


 Wachezaji wa timu ya Yanga wakiomba dua katika moja ya mechi za na watani wao Simba


          Kikosi kamili cha wakali wa msimbazi, Simba Sports Club ya jijini Dar-es-salaam


Kikosi kamili cha wakali wa mtaa wa jangwani, Dar Young African (Yanga) ya jijini Dar-es-salaam.

Macho na masikio ya mashabiki wote wa soka Tanzania kesho yataelekezwa katika uwanja wa taifa ambapo watani wa jadi Simba na Yanga watakuwa wakikpepetana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya vodacom Tanzania bara. Simba wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwatandika watani wao hao mabao mawili kwa sifuri (2-0) katika mechi ya ngao ya hisani ambayo ilikuwa ni ishara ya kufungua msimu mpya wa ligi hiyo..papo hapo Yanga wao wataingia na matumaini wakiwa na kocha wao mpya PAPIC baada ya kimtimua kocha wa awali SAM TIMBE na wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja kwa sifuri katika mechi yao iliyopita huku Simba wao wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao mawili kwa sifuri katika mechi yao iliyopita ya ligi….Dakika 90 zitakazosimamiwa na mwamuzi OdenMbaga hapo kesho ndizo ziatakazoamua nani ni nani kati ya Simba na Yanga….YETU MACHO

KENYA NA OPARESHENI YA KUWATOKOMEZA AL-SHABAB

 Baadhi ya wanamgambo wa Al-Shabab wakiwa na siraha mikononi tayari kwa ajili ya mapambano


 Wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabab wakiwa katika moja ya misafara yao ya kila siku


 Wanamgambo wa kukundi cha Al-Shabab wakiwa wamepumzika, kenya wanahaha usiku na mchana kuwatokomeza wanamgambo hawa


Wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabab wakiwa katika mafunzo ya jinsi ya kutumia na kulipua makombora kama wanavyoonekana katika picha. Kenya wanahaha usiku na mchana kuwatokomeza wanamgambo hao kufuatia muendelezo wa mashabulio ya mabomu katika jiji la nairobi ambayo yanaripotiwa  kufanywa na wanamgambo hao.


Majeshi ya Kenya yameendelea na msako wa kuwasaka wanamgambo wa kikundi cha Al-shabab ambacho kinasadikika kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kufuatia kutekwa nyara kwa raia wa kifaransa aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la misaada la umoja wa mataifa. Oparesheni hiyo ambayo inaendeshwa na Kenya katika nchi ya Somalia imefuatiwa na utata baada ya raisi wa Somalia kudai kuwa hawakutoa ruhusa kwa Kenya kuendesha oparesheni ya kijeshi katika nchi hiyo na papo hapo ikafuatiwa na mashambulio matatu katika jiji la Nairobi ambapo katika shambulio la jana basi lililokuwa na maafisa wa elimu wa Kenya waliokuwa katika harakati za kusimamia mitihani ya nchi hiyo lilishambuliwa mpakani mwa Kenya na Somalia na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine kujeruhiwa vibaya…swali ambalo watu wengi bado wanajiuliza ni je Kenya watawaweza Al-shabab au wamewasha moto ambao utawashinda kuuzima?..pamoja na hayo ufaransa imeahidi kuisaidia Kenya katika oparesheni hiyo ya kutokomeza kikundi hicho cha wanamgambo wa Al-shabab

Thursday, October 27, 2011

SIMBA NA WASIWASI JUU YA ODEN MBAGA

          Kikosi kamili cha wababe wa mtaa wa msimbazi,SIMBA S.C ya jijini Dar-es -salaam



 Tamko la msemaji wa simba Ezekiel Kimwaga juu ya wasiwasi wao juu ya mwamuzi wa mchezo kati yao na watani wao wa jadi Yanga ya jijini Dar-es-salaam utakaopigwa katika uwanja wa taifa jumamosi hii

Sunday, October 23, 2011

OLD TRAFFORD YAZINDULIWA NA MANCHESTER CITY FC


Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Kun Aguero akishangilia goli alilolifunga dhidi ya timu ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford. Man City waliitandika Man Unt 6-1

                                  Kocha wa Man City Robert Mancin akifuatilia mtanange huo




Hatimaye wasiofungika Man Unt wamezinduliwa rasmi na majirani zao Manchester City kwa kipigo cha mabao 6 kwa 1 katika uwanaja wao wa nyumbani wa Old Trafford. Mario Balloteli ama Super Mario ndiye aliyeongoza mauaji hayo ya Man U kwa kutupia goli 2, huku Aguero,Dzeko, Silva nao wakichangia ushindi huo mnono wa Man City dhidi ya Majirani zao hao. kwa ushindi huo Man City wameiidhihirishia United kuwa wao si tu majirani zao bali ni wapinzani wa namba moja katika mbio zao za kuutetea ubingwa wa ligi hiyo yenye msisimko zaidi ulimwenguni. pia mechi hiyo ilishuhudia John Evans wa Man U akitolewa nje kwa  kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Super Mario........

WIZARA YA ARDHI NA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA







MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA YA WIZARA YA ARDHI
MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA (MB.), WAKATI WA UFUNGUZI WA MAONESHO YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO  YA MAKAZI  KUANZIA TAREHE 22 SEPTEMBA HADI 25 SEPTEMBA, 2011 KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM
Kaimu Katibu Mkuu, Ndg. Maria Bilia,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki,
Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam,
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
Wastahiki Mameya wa Manispaa zote za Dar es Salaam,
Ndugu Viongozi na Watendaji wa Halmashauri Nchini
Ndugu Viongozi wa Taasisi na Mashirika Mbalimbali
Wenyeviti wa Bodi Mbalimbali,
Wakurugenzi, Maafisa  na Watendaji wa Wizara,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Ndugu Wadau wa Sekta ya Ardhi , Nyumba na Makazi, awali ya yote natoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha sisi wote kuwepo hapa siku ya leo. Nawashukuru kwa kuitika kuja kushiriki kwa kujionea yale ambayo yanayofanyika katika sekta ya Ardhi, Nyumba na Makazi nchini kwetu tangu tupate uhuru. Kufika kwenu hapa ni tafsiri sahihi ya kutambua kuwa hii sekta ipo kwa ajili ya watu, na ni watu wote; wazee, watoto na wanawake, wote ni wadau kwa sababu hakuna maisha pasipo makazi na hakuna maendeleo pasipo Ardhi. Ardhi, Nyumba na Makazi kwa ujumla ni mahitaji ya kwanza mtambuka katika kupanga   shughuli au mkakati wowote wa maendeleo.
Ndugu Wananchi, Wizara yangu ilikuwa ikiunganishwa kimuundo na sekta mbalimbali tangu uhuru kama misitu, maji, madini na utalii hadi mwaka 2001 yalipofanyika mabadiliko na kuitwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mpaka sasa.
Pamoja na mabadiliko mbalimbali,Wizara yangu imekuwa na majukumu mbali mbali katika kuendeleza sekta mama ya ardhi nchini, yakiwemo kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi pamoja na Sheria zinazohusu sekta ya ardhi na nyumba, kusimamia na kufanya shughuli za upimaji ardhi na uandaaji ramani, kuendeleza makazi, kusimamia na kufanya shughuli za uthamini, kusimamia na kufanya shughuli za usajili wa hati za kumiliki ardhi, kupanga na kusimamia matumizi bora ya Ardhi, kufanya utafiti wa vifaa vya ujenzi wa nyumba bora, Kupanga na kusimamia maendeleo ya miji, kusimamia shughuli za upimaji ardhini na majini na kufanya utafiti wa vifaa vya ujenzi wa nyumba bora
Ndugu Wananchi, Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa upande wa Wizara yetu yanaanza rasmi leo tarehe 22 Septemba, 2011 na yanamalizika tarehe 25 Septemba, 2011. Hata hivyo, maadhimisho haya ambayo yanaendelea hadi Desemba yanalenga kutangaza mafanikio yaliyofikiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara tangu Desemba 1961 hadi sasa.  Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni kuwa “Tumethubutu kuwa na ardhi ambayo ni mtaji na ni mali, Tumeweza kuiendeleza na Tunazidi kusonga mbele katika kuendeleza ardhi yetu kwa manufaa ya Watanzania wote”
Ndugu wananchi, wakati leo tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, takwimu mbalimbali zinazotokana na tafiti zinazofanywa na taasisi za kimataifa zinaashiria kuwa katika bara la Afrika, Asia, Marekani ya Kusini (Latin America) na Carribeani tunahitaji mikakati ya ziada ili kuweza kukabiliana na suala la makazi kutokana na kasi ya kuongezeka kwa watu kuhamia mijini.
Mfano kufikia 2050 zaidi ya watu bilioni sita ambayo ni theluthi mbili ya wakazi wote duniani watakuwa wanakaa mijini.
Ripoti na maazimio ya Agenda ya Makazi, Azimio la Vancouver na makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi, Azimio Na.56/206 vyote vinatahadharisha tuwe makini na mipango ya makazi.
Ili kufanisha haya tunahitaji kuwa na ushirikiano wa karibu katika kupanga matumizi ya ardhi ili kuweza kuendelea na matumizi mengine ya ardhi.
Hata hivyo Wizara ya Ardhi inajivunia mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hii. Wizara ilianza kama Idara ya Ardhi na Upimaji mwaka 1957 ikiwa na idadi ndogo ya watumishi na majukumu machache sana. Iliendelea kukua na kubadilishiwa majukumu na jina kubadilika mara kwa mara kama mtakavyoona katika vipeperushi vilivyogawanywa. Leo tunaposheherekea miaka 50 ya uhuru, majukumu ya Wizara na Sekta ya Ardhi kwa ujumla yameongezeka na idadi ya watumishi imeongezeka sana hadi kufikia zaidi ya watumishi 1400 na bado hawatoshi kukidhi mahitaji yote ya Wizara na Halmashauri.
Ndugu wananchi, wakati Tanzania Bara inapata Uhuru wake mwaka 1961 Sekta ya Ardhi ilikuwa haichangii kwa kiwango kikubwa katika Pato la Taifa. Hii ilitokana na sabau kwamba ardhi ilikuwa haijaandaliwa mipango wala kupimwa. Hivi sasa maeneo mengi ya mijini yamepimwa na pato la taifa kutokana na ardhi limeongezeka kutoka Shilingi 650,000,000  kwa mwaka 1995/96hadi kufikia jumla ya Shilingi Bilioni 15.6 kwa mwaka 2010/11. Natoa wito kwa wananchi kupima maeneo yao ili kuongeza mapato yao binafsi na hata ya Taifa letu. Ardhi iliyopimwa ni mali na ni mtaji kwani inajulikana kwa urahisi kwa vile ina vielelezo vya kumilikiwa na mtu au asasi katika mfumo wa hati.
Ndugu wananchi, napenda kuwaeleza kuwa, umiliki wa ardhi kwa kuandikishwa ulianza toka wakati wa utawala wa Mjerumani . Hadi tunapata uhuru, watu waliokuwa wanamilikishwa ardhi kwa kusajiliwa walikuwa ni wageni peke yao. Wananchi walianza kumilikishwa ardhi baada ya uhuru ambapo mpaka sasa jumla ya miliki 739,712 za ardhi zimetolewa. Aidha, Wizara imeanzisha mpango wa kupima mipaka ya vijiji ambapo vijiji 11,260 vilipimwa na kutoa vyeti 7,510. Mpango huo uliwezesha kupima mashamba ya wananchi na kutoa hatimiliki za kimila. Hadi sasa jumla ya hati miliki za kimila 157,968 zimetolewa katika wilaya mbalimbali nchini. Utoaji wa vyeti vya vijiji unaendelea na vijiji vyote vilivyopimwa mipaka yake vitapata vyeti kabla ya kilele cha maadhimisho tarehe  9 Desemba 2011.
Ndugu wananchi, wakati tunapata Uhuru, Mwaka 1961, jumla ya hati 14,448 za kumiliki ardhi zilikuwa zimesajiliwa. Hati hizo zilikuwa zimetolewa katika maeneo ya kati ya miji na maeneo ya mashamba makubwa ya mkonge, kahawa, na chai yaliyokuwa yanamilikiwa na wageni. Baada ya Uhuru hadi sasa, kuna jumla ya hati milki 379,000 zilizosajiliwa na kutolewa kwa wananchi. Aidha, ili kurahisisha utoaji wa hati ofisi za Usajili zimeongezeka kutoka moja iliyokuwepo wakati wa Uhuru hadi kuwa na Ofisi za Usajili za Kanda 6 zilizoko Dar es Salaam, Mwanza, Moshi, Dodoma, Mbeya na Mtwara.  
Ndugu wananchi, huduma za upimaji ardhi hapa nchini zilianza toka miaka ya 1890. Ili kiumarisha fani hii, Serikali ilianzisha Halmashauri ya Wapima ambapo hadi sasa jumla ya wapima ardhi 225 wamesajiliwa. Pia, kwa kushirikiana na Halmashauri nchini, jumla ya viwanja 900,000 na mashamba 20,883 vilipimwa katika miji mbali mbali nchini. kwa kutumia mfuko wa upimaji na mradi wa viwanja mijini. Mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 iliyopita ni pamoja na kubadilisha mfumo wa utayarishaji ramani kutoka analojia kwenda dijitali, kutumia picha za satelaiti badala ya picha za anga kuhuisha ramani, kuanzishwa kwa vituo 5 vya upimaji wa moja kwa moja kwa kutumia satelaiti na kuweka alama mpya 1,327 za msingi za upimaji ardhi, kukamilisha upimaji wa mipaka ya eneo la kiuchumi katika Baharini (EEZ).  Aidha, wizara imeanzisha kanda 5 za ukaguzi na uidhinishaji wa kazi za upimaji.
Hadi mwaka 2010 ramani zote zilikuwa zinaidhinishwa Dar es Salaam. Ili kurahisha upimaji wizara ina mango wa kuanzisha Kituo cha kupokea picha za satellite hapa nchini kitakachojengwa mjini Dodoma.
Ndugu wananchi, upangaji na uendelezaji wa miji ulianza toka enzi ya ukoloni. Wakati tunapata Uhuru, kulikuwepo na Miji 31. Baada ya miaka 50 kuna Miji rasmi 118, Vituo vya biashara (Minor Settlement/trading Centres) zaidi ya 200 .Kati ya Miji hiyo Majiji ni 5, Manispaa 18, Miji 6 na Miji midogo 95. Aidha, katika miaka ya sitini Mji uliokuwa na Mpango Kabambe ni Dar es Salaam pekee, Miji mingine ilikuwa na Mipango ya kina (Planning Schemes). Hivi sasa Miji ya Mikoa 19 imeandaliwa Mipango ya muda mrefu (Master Plans) na Miji midogo 48 imeandaliwa Mipango ya muda mfupi (Interim Land Use Plans). Sambamba na hilo kuna Mipango ya Uendelezaji Upya ya Makazi (Redevelopment Schemes) ambayo imeandaliwa katika miji mikuu ya Mikoa 17 (Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi, Iringa, Sumbawanga, Lindi, Mtwara, Kigoma, Morogoro, Singida, Shinyanga, Musoma, Tabora na Songea) kwa nchi nzima. Mipango ya kina ya Mipango ya Miji iliyoandaliwa nchi nzima kuanzia mwaka 1960 hadi 2011 ni 4,363 ambayo imeweza kuzalisha viwanja 1,802,015 kwa matumizi mbalimbali ya Miji. Juhudi za kuendelea kupanga zitapanuliwa mpaka ngazi ya kijiji ili kuleta ufanisi katika matumizi endelevu ya ardhi nchini.
Ndugu wananchi, kutokana na ongezeko kubwa la watu katika miji yetu, ujenzi wa makazi umekuwa ukienda kwa kasi kubwa kulinganishwa na kasi ya upangaji miji. Hali hii imesababisha ongezeko kubwa la makazi holela mijini. Katika jitihada za kuboresha makazi nchini, ulianzishwa Mpango wa kurasimisha ardhi na nyumba. Hadi Juni 2011, jumla ya nyumba 301,961 zilitambuliwa kwenye maeneo yaliyojengwa bila kupangwa katika miji ya Mwanza, Dar es Salaam, Moshi, Dodoma na Tanga. Kati ya nyumba zilizotambuliwa, jumla ya leseni 92,565 zilitolewa. Ili kukabiliana na tatizo hili, Serikali itaongeza juhudi za kupanga miji na kuwezesha upatikanaji wa makazi yaliyopangwa mjini kukidhi mahitaji. Natoa wito kwa wananchi kacha kujenga kwenye maeneo yasiyopimwa.
Ndugu wananchi, maendeleo ya nyumba yanajumuisha upatikanaji wa ardhi, miundombinu, upatikanaji wa fedha, upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na nguvu kazi. Hali ya nyumba na upatikanaji wa miundombinu imebadilika sana tangu mwaka 1961. Kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita tangu kupata uhuru, Serkali imekuwa na sera stahiki ya uwezeshaji (enabling approach) wananchi kujijengea nyumba, kuwahakikishia milki salama, kurekebisha na kujenga miundombinu katika makazi yaliyojengwa bila kuzingatia mipango miji lakini ambayo hayakuendelezwa kwenye maeneo hatarishi kimazingira. Licha ya ongezeko kubwa la watu mijini kutoka watu takriban laki 4.5 mwaka 1961 walikuwa wanaishi mijini hadi watu wanaokadiriwa kuwa milioni 15 leo hii. Sera hii imeepusha tatizo la kuwa na watu wasio na makazi kabisa.
Kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa wananchi wameweza pia kuchangia katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, umeme, elimu, afya na uondoshaji wa maji taka na taka ngumu. Kutokana na juhudi za pamoja leo hii, asilimia 77 ya kaya zilizopo mijini zinapata maji kutoka kwenye vianzo salama (bomba au kisima).
Serikali imeweza pia kuboresha hali ya makazi kwa kujenga miundombinu, barabara, mifereji ya maji ya mvua, umeme, maji na mfumo wa uondoshaji wa taka katika miji mbalimbali, ukiwemo ule wa Urban Sector rehabilitation Project uliotekelezwa katika miji ya Arusha, Moshi, Morogoro, Tanga, Mbeya, Iringa na Mwanza. Mradi mwingine ni ule wa Community Infrastructure Upgrading Programme unaondelea kutekelezwa Jijini Dar es Salaam katika makazi 30 tofauti ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 200,000. Serikali inaendelea kuboresha sera na sheria ili kuimarisha mazingira ya kuwezesha wananchi kuwa na nyumba na makazi bora zaidi ikiwa ni pamoja na kuvutia benki za biashara na vyombo vingine vya fedha kutoa mikopo ya nyumba.
Ndugu wananchi, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni Shirika la kwanza kuanzishwa nchini baada ya uhuru wa Tanganyika 1962. Shirika lilianzishwa kwa lengo la kuwapatia wananchi makazi bora kutokana na Serikali kuthamini makazi bora kuwa ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu. Katika kipindi cha miaka 50, Shirika limejenga jumla ya nyumba 17,168 za makazi, upangishaji na majengo ya ubia na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kutekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo, Shirika lina mpango wa kujenga 15,000
Ndugu wananchi, katika jitihada za kutatua migogoro ya ardhi na nyumba, Serikali ilitunga Sheria ya mahakama za Ardhi iliyowezesha kuundwa kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 39 katika ngazi ya Wilaya na Mkoa. Hadi sasa, umeanzishwa mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi na nyumba kuanzia ngazi ya kijiji. Kuanzishwa kwa mabaraza haya kumewezesha mashauri ya ardhi na nyumba kushughulikiwa kwa muda mfupi, kusikilizwa na kuamliwa. Toka Mabaraza haya yaanzishwe mwaka 2004, jumla ya mashauri yaliyoamuliwa ni 39,000 kati ya mashauri 54,760 yaliyofunguliwa. Idadi hii ni kubwa ukilinganishwa na mashauri yaliyowahi kuamuliwa hapo awali.
Ndugu wananchi, ili kuwa na matumizi ya ardhi endelevu mijini na vijijini, Serikali iliunda Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi mwaka 1983. Tangu Tume ilipoundwa,  imewezesha uaandaaji wa wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya 38 nchini. Aidha katika kipindi hicho, Tume kwa kushirikiana na Halmashauri za vijiji imefanikisha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 1,000 katika wilaya 78 kwenye mikoa 20 ya Tanzania bara. Pia Tume imeandaa Mpango wa Taifa wa matumizi ya ardhi kwa miaka 30 ijayo, ambao unabainisha matumizi ya ardhi kwa kila kipande cha ardhi nchini. Mpango huu unagusa sekta zote zinazotumia ardhi kama vile maji, barabara, kilimo, mifugo, mali asili, nishati na madini n.k
Ndugu wananchi, pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50. Sekta ya ardhi na nyumba inakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni chachu ya mafanikio ya sekta katika miaka 50 ijayo. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wananchi na wadau kuhusu Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu masuala ya Ardhi, kuwepo kwa migogoro mbalimbali ya ardhi inayokwamisha kuwapa wananchi hati za kumiliki maeneo yao, kasi ndogo ya kuanzisha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ilikinganishwa na idadi ya Wilaya ambazo zinahitaji huduma hii, kuwepo kwa ongezeko la ujenzi holela mijini ambapo asilimia zaidi ya sabini ya makazi mijini wanaishi katika maeneo yasiyopimwa, riba kubwa ya asilimia 17-18 inayotozwa na vyombo vya fedha vinavyotoa mikopo ya nyumba, kunakosekana vivutio vya kushawishi sekta binafsi kuwekeza kwenye sekta ya nyumba na kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi na hivyo kufanya gharama za ujenzi kuwa juu n.k.
Ndugu wananchi, ili kukabiliana na changamoto hizo wizara inayo mikakati na mipango thabiti ambayo itatekelzwa. Mipango hiyo inapatikana kwenye vipeperushi mbalimbali vilivyosambazwa na katika mpango ya serikali wa miaka mitano.
Ndugu wananchi, naona niishie hapa na niwaalike kuungana nasi katika maonesho haya ili muone kazi za wizara na mabadiliko mbalimbali ya kiteknolojia. Kwa nafasi hii naomba kuwashukuru tena kuungana nasi katika siku hii ya ufunguzi. Lengo la juhudi zote hizi ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu uendelezaji wa miji, nyumba na dhana ya ardhi ni mtaji kutoka katika hali ya mtaji mfu kwa la kupunguza umasikini wa mtanzania mmoja mmoja hadi katika kuchangia pato la taifa.
Sasa kwa heshima na taadhima naomba nifungue rasmi maonesho haya na niwakaribishe wote kutembelea mabanda na kujifunza mambo mbalimbali ya sekta ya ardhi. Kauli Mbiu ya Kitaifa ya maadhimisho haya ni “Tumethubutu kuwa na ardhi ambayo ni mtaji na ni mali, Tumeweza kuiendeleza na Tunazidi Kusonga Mbele katika kuendeleza ardhi yetu kwa manufaa ya watanzania wote.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA

Saturday, October 22, 2011

ISRAEL AND PALESTINE DEMANDS FOR PEACE

                                         Mahamoud Abbas, Palestine's prime minister

                           Barack Obama,President of The United States of America

 

Benjamin Netanyahu, Israel's Prime Minister

The issue of peace in the Middle East currently is the most hot and intense issue all over the world especially the conflict between Israel and Palestine. Hope for peace in this region rises following the signing of the Refugees exchanging agreement between the government of Israel and Hamas.
             The conflict between Israel and Palestine can be traced back during the 1947 United Nations Resolution which was passed to initiate the creation of Jewish state within Palestine. This led to the 1948 Arab-Israel war.
            Certain portions which were taken by Jews after they won the war are very important for the religious issues to the Muslim like the some parts of East Jerusalem where the AL-AQSA mosque is situated, but also the Wailing Wall

PALESTINIANS and the conflict
They feel that they are not free people because Israel soldiers stop them at check points between cities and therefore they must gain Israel’s approval each day to go to work, also they have less access to water.

PALESTINIANS DEMANDS FOR PEACE
i.                    a separate Palestinian state with 1967 boarders
ii.                  Palestinian control of East Jerusalem
iii.                Ending Israel occupation over Palestinian territory
iv.                Freedom of Palestinian refugees to return to their homeland

ISRAEL and the conflict
They view Palestinians militants as the terrorist who will not compromise to gain peace

ISRAEL DEMANDS FOR PEACE
i.                    Palestine boarders that ensures continuing Israel security from Palestine attack not the 1967 boarders
ii.                  Israel control of all Jerusalem
iii.                Enough Israel control within Palestinian to allow Israel to destroy terrorist attack
iv.                Prevention of Palestinian refugees from returning to their home land.

Wednesday, October 19, 2011

READ THIS POEM AND REFLECT IT TO THE CURRENT SITUATION IN TANZANIA


PEASANT BY SYL-CHEYNEY COKER

The agony: I say their agony
The agony of imagining their squalor but never knowing it
The agony of cramping them in roach infected shacks
The agony of treating them like chattel slaves
The agony of feeding them abstract theories they do not understand
The agony of their lugubrious eyes and bartered soul
The agony of giving them party card but never party support
The agony of marshalling them on Election Day but never on barguest nights
The agony of giving them malliferous words but mildewed bread
The agony of their cooking hearths damped with unuse
The agony of their naked feet on the hot burning tarmac
The agony of their children with projectile bellies
The agony of long miserable nights
The agony of their thatched houses with too many holes
The agony of erecting hotels but being barred from them
The agony of watching the cavalcade of limousines
The agony of ground state balls for God knows who
The agony of those who study meaningless “ism” in incomprehensible language
The agony of intolerable fees for schools but no jobs in night
The agony of it all I say the agony of it all but above all the damn
Agony of appealing to their patience
Africa bewares! Their patience is running out!!

TANESCO KWANINI WAILIPE DOWANS BILIONI ZETU 94?

Jengo la makao makuu ya shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) lililopo ubungo jijini Dar-es-salaam

      Kwa ufahamu wangu finyu ukiniuliza kwa nini TANESCO wailipe DOWANS Tanzania Limited bilioni zetu 94 ntakupa majibu haya
                        1..sheria zetu butu juu ya makampuni ya wageni na wawekezaji
                        2..Tanesco walikubali kusaini mkataba wenye kifungu kinachowafunga kuwa maamuzi ya ICC ndo ya mwisho na hayatakuwa na rufaa na bila kufikiria maamuzi gani yatafanywa na ICC iihali wanajua kuwa DOWANS ni kampuni tata.

     Tanesco ambao waliingia mkataba na Dowans Tz limited ambayo ilirithi mkataba toka kwa Dowans Holdings SA ya Costa Rica ambayo ilirithi mkataba huo toka kwa Richmond Development, walikuwa wanajua kabisa kuwa wanaingia mkataba na kampuni ambayo tayari ina utata na imeshaisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi

Chadema wameamua kuipa serikali siku 30 tangu octoba 8 kusitisha malipo hayo kwa Dowans vinginevyo watalipeleka suala hilo kwa wananchi walifanyie maamuzi, hili linakuja baada ya mahakama kuu ya Tanzania kuiamuru Tanesco iilipe Dowans kufuatia kuwepo kwa kufungu ambacho kilikataza chombo chochote cha sheria kuingilia au kutoa maamuzi juu ya mkataba huo, kwamba maamuzi ya ICC ( mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ) kuwa ndio yatakuwa ya mwisho na hakutakuwa na kukata rufaa…kusainiwa kwa mkataba huo inamaanisha kuwa Tanesco walikuwa na imani kuuubwa na ICC kiasi cha kuamini kuwa maamuzi yake yatakuwa ya haki lakini leo maamuzi hayo yanatupa kizungumkuti watanzania…
 Maswali ya kujiuliza ni haya
1.      Tanesco walifanya maamuzi ya kizalendo?
2.      Sheria zetu zina utetezi gani juu ya maamuzi yaliyofikiwa?
3.      Nini kauli na msimamo wa serikali juuu ya malipo hayo, ikiwa baadhi ya watendaji wa serikali wanakili kuwa dowans ni wahuni?
4.      .Nini wamefanywa mpaka sasa watendaji wa taneco waliopelekea kizungumkuti hiki?
Binafsi sitamani hata kidogo kushuhudia Dowans wakilipwa mabilioni haya ya wavuja jasho..msimamo wa Samwel Sitta akiwa ni mtendaji wa serikali kwanini usiwe msimamo wa wenzie waliomo katika serikali hiyo hiyo na hatimaye kuwa msimamo rasmi wa serikali?

Tuesday, October 18, 2011

TEMBO WATUMIKA KUZALISHA UMEME

Moja kati ya tembo ambao kinyesi chao hutumika kuzalisha biogas kwa ajili ya kuzalisha umeme

Tembo wenye asili ya India wanatumika kuzalisha umeme katika moja ya vituo vya wanyama maarufu kama “zoo” iliyoko huko munich ujerumani. Vinyesi vya tembo hao hukusanywa katika makontena makubwa matatu ambapo kila kontena lina uwezo wa kuchukua mpaka cubic mita 100 za vinyesi hivyo na kisha kutengenezwa gesi inayotokana na mabaki  au taka za wanyama hao maarufu kama “ Biogas” ambayo hutumika kuzalisha umeme ambao hutumika katika kituo hicho

Saturday, October 15, 2011

LIVERPOOL 1 MANCHESTER UNITED 1

Kiungo wa klabu ya soka ya liverpool ya uingereza Steven Gerrad akichuana na kiungo wa manchester united Darren Fletcher katika mchezo uliopigwa leo kwenye uwanja wa Anfield na timu hizo kutoka sare ya 1-1

Presha za mashabiki wa klabu za liverpool na manchester united hatimaye zimeshuka baada ya mchezo kati ya wapinzani hao wawili  katika ligi kuu ya uingereza kumalizika kwa sare ya gori moja kwa moja.Liverpool walianza kulisabahi lango la manchester united kufuatia faulo ya Gerrad na Giggs kuukwepa mpira, mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico Javier Hernandez " Chicharito" aliisawazishia manchester unietd kwa kichwa kufuatia mpira wa kona........

Friday, October 14, 2011

KUFUNGIWA KWA ROONEY NI PIGO.......CAPELLO

                                   Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello


                   Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney aimkwatua mlinzi wa Montenegro Miodrag Dzudovoic, faulo iliyopelekea kupewa kadi nyendu

Kocha wa timu ya taifa ya uingereza fabio capello amesema kuwa kufungiwa mechi tatu kwa mshambuliaji wa timu hiyo katika michuano ijayo ya ubingwa wa mataifa ya ulaya ni pigo kwa timu hito yenye hamu kubwa ya kuupata ubingwa huo. Rooney atakosa mechi zote tatu za hatua ya makundi kufuatia kufungiwa michezo mitatu na shirikisho la soka barani ulaya ( uefa)..capello amezipata taarifa hizo akiwa mapumzikoni kwao italia.

TEVEZ AREJEA MANCHESTER CITY

    Mshambuliaji wa klabu ya soka ya manchester city ya nchini uingereza Carlos Tevez akishuka kutoka garini mwake mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mazoezi " carrington" baada ya     kumaliza adahabu yake.

Mshambuliaji wa kimataifa wa argentina na klabu ya soka ya manchester city amerejea katika kikosi hicho kuendelea na mazoezi baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo cha wiki mbili kufuatia kutuhumiwa kususia mchezo wa ligi ya mabingwa ya ulaya dhidi ya wababe wa ujerumani bayern munich

Thursday, October 13, 2011

TUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA KUSISITIZA UTAWALA BORA WENYE KUZINGATIA MISINGI YA KATIBA

                                      Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere




              Ijumaa Octoba 14 ya kila mwaka watanzania wote kote duniani huungana pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa taifa hili hayati Julius Nyerere. Ni siku ambayo hutukumbusha majonzi tele yasiotarajiwa kuja kukauka kamwe...ni siku ambayo baba wa taifa aliaga dunia katika hospital ya Mtakatifu Thomas huko London Uingereza


             kumbukumbu hizi huambatana na shughulu mbalimbali zenye lengo la kuenzi fikra, wosia na falsafa za baba wa taifa. Binafsi ningependa kuwasisitiza watanzania wenzangu tuenzi na kudumisha falsafa za baba wa taifa kwa kusisitiza utawala bora wenye kufuata misingi ya haki, utawala bora na katiba japokuwa kuna mapungufu lukuki katika katiba tuliyonayo kiasi cha kulia kila iitwayo leo kufanywa haraka kwa mchakato wa kuandika katiba mpya yenye manufaa na maslahi kwa watanzania walio wengi.


               Mwalimu Nyerere alilinda na kuiheshimu katiba kiasi cha kila mtanzania kuridhika na utawala wake, ni katiba hii hii yenye mapungufu lukuki ambayo baba wa taifa aliiheshimu na kuilinda kiasi cha watanzania kukubali utawala wake. hakuhubiri udini hata kidogo kwa sababu alijua ni kinyume na katiba, alisisitiza haki, usawa na haki  baina ya raia wote wa  Tanzania.


            Ni jinsi gani viongozi wetu wa leo wanaongozwa na katiba na sheria ndilo swali kubwa tunalopaswa kujiuliza na kutafuta majibu........kwa mfano, katiba inatamka wazi katika ibara ya 3 (1) kuwa "jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.". je kuna uhalisia katika mifumo ya kututawala iliyojengwa na viongozi wetu wa sasa ya kuwa kuna demokrasia?..je si ni hawa hawa baadhi ya watawala wetu wanaoamua kutugawa kwa misingi ya udini?

        Vile vile katiba inatamka wazi katika ibara ya 13 ibara ndogo ya 6, kifungu (a) ".kwa madhumuni ya kuhakikisha haki na usawa mbele ya sheria, mamlaka ya nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia msingi kwamba;...wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na mahakama au chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika.". Je ni watanzania wangapi ambao bado haki na usawa mbele ya vyombo vya sheria ni ndoto kwao??

Wednesday, October 12, 2011

Ikulu Mawasiliano: HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WANANCHI, TAREHE 30 SEPTEMBA, 2011

Ikulu Mawasiliano: HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WANANCHI, TAREHE 30 SEPTEMBA, 2011

CLEVERLEY ASAINI MKATABA MPYA MAN UNTD

          Thom Cleverley wa Manchester united akishangilia moja ya magori aliyoifungia timu hiyo katika moja    ya michezo aliyoichezea
         Thom Cleverley akikokota ndinga katika moja ya michezo aliyoichezea timu ya taifa ya England ya vijana wenye umri chini ya miaka 21.


               Kiungo wa klabu ya manchester united ya Uingereza Tom Cleverley amesaini mkataba mpya utakaomuweka  katika klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kwa muda wa miaka minne zaidi na hivyo kuendelea kuwepo katika kikosi hicho cha mashetani wekundu mpaka mwaka 2015


                     Cleverley mwenye umri wa miaka 22 alizaliwa tarehe 12.agosti 1989 huko Uingereza. Akiwa na klabu hiyo ya manchester united Cleverley kapata mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwemo katika kikosi cha kwanza cha mashetani hao, kuitwa katika timu ya taifa ya taifa hilo ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 na pia timu ya taifa ya wakubwa.


Kwa sasa Cleverley bado yuko nje ya uwanja akisumbuliwa na maumivu ya mguu baada ya kuvunjika katika mchezo dhidi ya Bolton Wonderers ambapo Man utd waliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Monday, October 10, 2011

FAINALI BSS SECOND CHANCE OCTOBER 14.

Mkurugenzi mtendaji wa Benchmark Production Rita Poulsen akiwa na wasanii kumi walioingia kwenye kumi bora ya shindano la kusaka vipaji la bongo star search ambalo lilipewa jina la BONGO STAR SEARCH SECOND CHANCE, ambalo fainali yake inatarajiwa kuafnyika katika ukumbi wa Diamond jubilee siku ya ijumaa tarehe 14 mwezi huu wa kumi
           

                 Wasanii wanne wanatarijia kupanda katika steji ya ukumbi wa diamond Jubilee kuchuana kuwania nafasi ya kwanza katika kinyang'anyiro hicho ambapo ni pamoja na mwanadada Bella Kombo, Haji Ramadhani, Rodgers Lucas na Waziri Salum. ambapo mshindi wa kwanza anataraija kuondoka na kitita cha takribani milioni 55 za kitanzania...wakati huo huo msanii Mr Flavour kutoka Nigeria anataria kuzipamba fainali hizo za aina yake katika tasnia ya muziki wa Tanzania siku hiyo ya ijumaa.

Sunday, October 9, 2011

Christiano Ronaldo awakebehi mashabiki wa Barcelona

Kiungo mshambuliaji machachari wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Christiano Ronaldo ameendeleza mbwembwe na majigambo yake safari hii akiwalenga zaidi mashabiki wa Barcelona ambao ndio mahasimu wao wakubwa pale aliposema ya kwamba..."kila anayeujua mpira na anayependa mpira basi hupenda kumuona na kumtazama yeye akicheza ikiwamo mashabiki wa Barcelona...."

Mikakati hii ya 1995 haikupunguza mgao wa umeme?

Mnamo mwaka 1995 serikali iliamua kutekeleza mipango ifuatayo kwa ajili ya kupunguza mgao wa umeme  nchini..


  • kukarabati jenereta zote za dizeli ambazo zilikuwa hazitumiki katika mikoa ya Arusha, Mara, Tabora, Mbeya, Mwanza na Dodoma..serikali ililipatia shirika la umeme nchini TANESCO fedha kwa ajili ya kazi hii
  • kukamilisha mradi wa umeme wa pangani  falls
  • kuanzisha mradi wa dharura wa kujenga mtambo wenye nguvu ya kuzalisha umeme wa kati ya MW 60 hadi 160, mtambo ambao awali ulitazamiwa kutumia mafuta ya dizeli, lakini hapo baadae ungetumia gesi kutoka songo songo
  • kuendelea na upanuzi wa matumizi ya makaa ya mawe kutoka machimbo ya kiwira, na umeme kutoka zambia ambao ulipatikana Mbozi.
  • Ujenzi wa mradi wa umeme wa Kihansi mkoani Morogoro
  • Utafiti kuhusu uwezekano wa kuunganisha gridi ya taifa na gridi za umeme za  nchi za Afrika Mashariki na Afrika ya kati kuongeza nguvu zaidi.










Ibara hii bado haijawafikia maskini..

katika katiba ya mwaka 1977 ya jamhuri ya muungano wa tanzania, ibara ya 13, ibara ndogo ya 6, kifungu (a).kwa madhumuni ya kuhakikisha haki na usawa mbele ya sheria, mamlaka ya nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia msingi kwamba;...wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na mahakama au chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kuopewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika..

uganda washindwa kufunzu michano ya mataifa ya afrika mwakani

pamoja na kucheza katika uwanja wa nyumbani, timu ya taifa ya uganda..(the cranes),ilishindwa kufunga bao hata moja katika uwanja wa nelson mandela stadium na hivyo kushindwa kufuzu kwa ajili ya mashindano ya mataifa huru ya afrika hapo mwakani..uganda ilikuwa ikihitaji pointi tatu au ushindi wa namna yeyote ile mbele ya kenya ili iweze kufuzu kwa ajili ya michano hiyo.....
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...