KUMBUKUMBU ZANGU .... FREDY JULIUS
KWA AJILI YENU KINA MAMA EDITHA WATANIKAMATA SANA NA SAMSON MWIGAMBA
Kuna vitu
navikumbuka katika maisha yangu, katika muktadha wa historia nimeona, nimesikia
na hata kutenda nimetenda mengi ijapokuwa sijala chumvi nyingi. Kumbukumbu
zangu zinaakumbuka mengi, namkumbuka Christian Luvanda kila ninaposikia msiba
na kweli naamini kuwa pengo la mtu huliziba mwenyewe, popote unapotutazama
Christian, pengo lako bado liko wazi hajapatikana bado wa kuliziba. Mioyo yetu
bado mizito, tunatamani kuamini kuwa umetutoka lakini tunashindwa kaka yetu, mioyo i radhi lakini
akili zinatukumbusha umuhimu wako kila tunapoamka. Akili mwamngu haujafutika na
sijui ni lini utafutika. Kila siku ninapoamka ni kama tarehe 31/01/2011 saa
kumi na mbili na dakika thelathini na sita asubuhi. Upumzike pema kaka yetu
mpendwa.
Nakukumbuka
kila niaposikiliza muziki wa hip hop, amani ya Tanzania sasa ipo kitanzini
wananchi wamepoteza matumaini ( citizens have lost their hopes). Tunatamani
kuendelea kucheka kama watanzania wamoja, baadhi yetu hatujui nini hasa kipo
nyuma ya pazia. Sitaki kukumbusha kuwa ulifaulu na haukuchaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza katika shule ya serikali wala kidato cha tano. Siku hizi
wanachaguliwa bila kufaulu.
Nakumbuka, ni
kweli mizinga tumechonga sisi asali wamelamba wao. Mramba asali kamaliza asali
mzingani, kasahau kuwa hata siku moja hakuchonga mzinga ili hali alichovya
chovya. Asali ni tamu na kila mtu
anaitamani, hata mimi pia, achilia mbali utamu wake lakini pia ni dawa. Mchana
na usiku naitaafuta, najua hata vidonda vya tumbo vinavyomtesa mama mzazi
hupoozwa na asali. Waonjaji wameimaliza tuliochonga mizinga tumebaki
kutazamana. Ndiyo ni kweli, mizinga tumechonga sisi asali wamelamba wao, kusoma
tumesoma sisi kufaulu wamefaulu wao, shule tumejenga sisi cha ajabu zimegeuka
kuwa za kwao, kodi tumelipa sisi huduma bora za kwao, tumevunjiwa nyumba zetu
sisi, tumehamishiwa pembezoni sisi, tumebebeshwa tofali na vifusi sisi,
barabara wanasafilia wao wakati sisi tukingoja katika msululu wa foleni. Ndiyo,
vyao vya kwao na vyetu vidogo wanavitaka pia bila aibu. Kusoma tumesoma sisi,
mitihani tumefanya sisi, matokeo wanayajadili wao.
Nakumbuka kuwa
ni chama cha mapinduzi kila ninapoona rangi ya kijani, ungetamani uchukie hata
kuyatazama majani na miti kwa mabadiliko haya ya tabia nchi, hakuna tena rangi
ya kijani, miti inapukutisha majani yake, ukame, ni rangi ya khaki kila sehemu
kama ulivopenda iwe. Nakumbuka harakati zako za mpakani na kombati yako ya
khaki. Najua baba, mama na mwana wote wako madarakani na mama amekuwa kaimu wa
baba na namsaidia majukumu ya kiofisi japokuwa katiba yetu iliyozeeka haimpi
fursa hiyo lakini ndiyo demokrasia yetu tuliyoichagua.
Nakumbuka
sikutaka kuwa Isack Newton, nikaamua kutoipenda fizikia na sikupata daraja la
kwanza, namkumbuka Sanga Michael alinisisitiza nisiache kusoma kemia, jeuri
zangu na kutotizama mbali sikumsikiliza, lakini nilikuja jua kwanini
nilitakiwan kusoma na sasa ninawahubiria wote umuhimu niliouona katika hili.
Angalau nakumbuka niliyojifunza katika biolojia, yananipa msaada na mwanga
katika katika maisha yangu ya kibinadamu.
Namkumbuka
profesa Shabani kila inapotajwa Udom, kuishi na kusoma hapa kumenifanya
niyaamini maneno ya wahenga kuwa “ Mungu siyo athumani “, na wala Mungu hawezi
kuwa shabani pia. Nakumbuka tarehe 12/06/2011 kila inapotajwa haki. Kumekuwa na
haki za mafungu, haki za wafungwa, haki za wanasiasa, haki za wanafunzi. Haki
itakuja kuwa na maana moja mbele ya sheria ijapokuwa ukubwa wa mafungu yake una
tofauti kubwa. Nakumbuka kuwa kuna harufu ya kifo kila inapotajwa haki.
Namkumbuka
Martin Luther King Junior kila ninapomsikiliza Barack Obama, kifo chake
kilishabihiana na haki na leo watu wanaiona haki aliyoihubiri. Hofu ya kifo
ilimtoweka mbele ya kilio cha haki, alijua atakufa na alijua kuwa atauawa kwa
aliyoyahubiri lakini ilimpasa kuhubiri haki. Kuna maisha yanavutia kama ya hawa
wanaharakati, kukiona kifo kilipo na kukifuata kwa nguvu zako zote ulizonazo.
Namkumbuka
Amina Chifupa kila ninapowaona mateja (wala unga), iliniuma nilipowaona wengi
mpaka katika viunga vya manispaa ya Iringa. Naona kuwa ujasiri wa mtu mara kwa
mara hurandana na kifo. Vaa ujasiri, sema kweli na hubiri kweli katika maisha
yako na jiandae na kifo na kama unaamini katika Mungu, fanya toba kila mara
unapokuwa umeamua kuhubiri haki.
Nalikumbuka
Azimio la Arusha na maneno ya hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere kila nipoona jahazi la Tanzania likienda mrama katika bahari hii ya
dhiki. Wanasema kuwa na rasilimali siyo utajiri kwa nchi, utajiri wan chi ni
uwezo wa wananchi kuzibadili rasilimali walizonanzo kuwa pesa. Najiuliza ni kweli
wasemayo? , najiuliza ni wapi hasa ni wananchi wa hii nchi wenye jukumu la
kubadili rasiimali hizi kuwa pesa? Maana ni kama kuna wananchi wa aina mbili,
wenye jukumu la kubadilisha rasilimali hizi kuwa pesa na wenye jukumu la
kufaidi pesa zilizobadilishwa kutoka katika rasilimali hizi za nchi.
Naamini rushwa
na ufisadi ni mapacha wa kufanana, sijalisahau bado azimio la Zanzibar. Wahenga
walisema “ usipoziba ufa utajenga ukuta”. Hakuna ugumu kuandaa tume kuchunguza,
hakuna ubaya kurudi nyuma na kujitathmnini, ugumu unakuja katika kufanya
maamuzi, ubaya unakuja katika kufanya maamuzi sahihi. Urahisi unatoka wapi
kumsema mwenzio kuwa ni mchafu ili hali wote mmezama katika shimo lililojaa
kinyeshi?. Kinyesi ni kinyesi na kitabaki kuwa ni uchafu hata kama wewe katika
utashi wako utabadili ukweli na kuona kuwa kinyeshi si kichafu na kuamua
kukila. Msafi na mchafu kwa hakika hawafanani, lakini hata wasafi kuna usafi wa
ndani na usafi wan je, pia hata wachafu kuna waliowachafu ndani mpaka nje na
kuna waliowasafi nje ndani wachafu. Ubaya wa unafiki ni kwamba humchafua mtu
nje ambako ndiko huonekana na watu na uzuri wa ukweli ni kwamba humsafisha mtu
ndani na kumpa amani.
Najua mafuta
ya ng’ombe mzee hayakatwi kwa kisu butu nab ado naamini hatua ya kwanza
kuelekea mafaniko ni uthubutu. Bado haijafutika akilini mwangu ziara ya
tarumbeta na injili ya mapacha watatu. Kivipi mwanadamu kutangaza utu ili hali
hausadiki?. Matendo ya muhubiri na maneno yapasa kweli kurandana ili kuleta
maana ya unachokizungumza kwa hadhira.
Najua sadaka
hutolewa kuunusuru utu wa mtu, sadaka itolewayo kuinusuru dhuluma siyo sadaka
ni kufuru. Iweje usimame mbele ya wanadamu kutangaza umetolewa sadaka?.
Maandiko ninayoyaamini yananifundisha kuwa sadaka ilikwishatolewa moja ya
mwanakondoo wa kweli aliyeshinda mauti. Umeunusuru utu wa mtanzania ama
umeinusuru dhuluma dhidi ya utu wa mtanzania . matendo machafu bado naamini
yanahitaji toba iliyo ya kweli, nakumbuka kufanya toba na kumuangukia Mungu
wangu kila ninpofanya kosa nab ado naamini hajanitoa nilikotoka ili nije
niishie hapa nilipofika sasa, safari yangu bado ni ndefu katika haya mapito ya
dunia.
Hawakumbuki
wanaendesha juu ya barabara ya Shaabani Robert, nakumbuka kuwa wanaendesha
katika nchi ya kusadikika. Mwanadamu anakuwa na matarajio gani pale anapokata
tawi la mti ambalo yeye mwenyewe amelikalia?. Bila shaka ni anguko kuu
litakaloacha vizazi vyake bila chochote cha kujivunia isipokuwa taabu, dhiki na
mahangaiko.
Namkumbuka
profesa Seith Chachage na Makuhadi wa Soko Huria wakati ninapoona mashirika ya
umma yakihudhuria sherehe za minada ya hadhara ya majengo ya ofisi zao kutokana
na kufilisika. Bado sijasahau namsoma profesa Issa Shimvji ndani ya Insha za
Wanyonge ili hali jasho laangu bado halinikauki na nawaona wanyonge wenzangu
wengi bado wakilisaka tonge. Bado nina uelewa ulio tata kila ninapozisoma insha
za Mabala wa Mabala, Hidaya taabu mjini, mpenziwe Frank naye bado anahaha na
kijiji. Bado sisahau kila asubuhi najiuliza swali ni vipi hili taifa change
lenye nusu karne nitalijenga.
Natamani kuwa
mwandishi kama Paschally Mayega, nimfundishe kila mtu yale niyawazayo akilini
ili name niwe mwalimu mkuu wa watu. Nimfundishe japo mtu mmoja kuwa uzalendo
haupatikani jkt bali mnaotaka kutupeleka ndiyo mmeukalia uzalendo tusiuone
katika macho yetu. Kivipi amani kwa ncha ya upanga na wananchi kila siku mtaani
wanaumia. Naikumbuka miezi mine ya njaa kila ninapokisoma cheti cha BAIR na
ninshaambiwa bila undugu sipati kazi wizara.
Namkumbuka
Daudi Mwangosi kila ninapowaona askari polisi, nakumbuka yaliyotokea Nyololo
njia panda iendayo shule ninayoipenda Igowole sekondari. Nasisimka, mwili joto
kali kama ninapigwa pasi. Maaskofu roho mkononi, uko wapi umoja na mshikamano
wa watanzania tuliojivunia?, uko wapi umojaa baba wa taifa aliotuachia.
Nakumbuka ulituunganisha kwa lugha ya Kiswahili, ukakipenda , ukakitangaza na
ukakiheshimisha kote barani afrika, lakini nakumbuka ulipigania umuhimu na
nafasi ya lugha ya kiingereza kubaki palepale kilipo.
KWA AJILI YENU KINA MAMA EDITHA WATANIKAMATA SANA NA SAMSON MWIGAMBA
NIANZE kwa kuwashukuru wasomaji wangu popote mlipo Tanzania.
Wengi mliwasiliana nami kuhususiana na yaliyonikuta. Baadhi nilijitahidi
kuwajibu lakini hatimaye simu, ujumbe mfupi wa simu na barua pepe zilizidi sana kiasi kwamba
sikuweza kuzijibu zote. Naomba niwashukuru sana walionipa pole, walionipongeza
na kunitakia mapambano mema hadi kieleweke.
Lakini kwa namna ya pekee, naomba ninukuu ujumbe wa rafiki
yangu na msomaji wangu wa siku nyingi, Dk. Masomo Lupembe. Yeye alisema:
“Mwigamba, shujaa huwa haambiwi pole! Kumwambia shujaa pole ni kumpunguza
makali na kumkatisha tamaa! Nichukue nafasi hii kukupongeza kwa yote
yaliyokukuta baada ya kuandika ule waraka kwa askari wote nchini. Kwenda
rumande kwa mpambanaji ni ushindi! Mwigamba umeshinda! Ujumbe umefika!
Nimepokea sms na kuzungumza na askari wa majeshi mbalimbali wanasema wako
pamoja na wewe! Songa mbele Mwigamba!”
Ninachotaka kuwaeleza wasomaji wangu ni kwamba wakati chura
anaruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine halafu wewe ukampiga teke akiwa
hewani unachofanya ni kumwongezea kasi ya kwenda na si kumuumiza.
Watawala wamenipiga teke nikiwa hewani naruka kusonga mbele
kwenye mapambano ya kuwapigania Watanzania kwa hiyo hawakuniumiza badala yake
waliniongezea kasi, hivyo nawashukuru wao na nawahakikishia siku nyingine
wataona matokeo ya kasi waliyonipa bila malipo.
Jumatatu wiki hii nilikuwa naangalia kipindi kimojawapo
kinachorushwa kwenye kituo cha televisheni cha Channel Ten kinachoitwa “Nchi
yetu”.
Katika kipindi hicho pamoja na watu wengi waliofika wa kada
mbalimbali ya maisha (isipokuwa watawala na mafisadi wao), alialikwa kwa
makusudi mama mmoja mfanyabiashara ndogo ndogo anaitwa Mama Editha.
Mama huyu anafanya kazi ya kukaanga na kuuza miguu, vichwa
na utumbo wa kuku. Biashara hii huweza kumwingizia kiasi cha shilingi elfu
mbili kwa siku. Nyumba anayokaa Keko Machungwa analipa shilingi elfu 20 kwa
mwezi. Ameachwa na mume na anaishi yeye na watoto wake ambao ni wakubwa lakini
hawajafikia umri wa kujitegemea na wengine wanasoma na ni yeye anawajibika
kuwalipia ada.
Biashara ya Mama Editha anaifanyia barazani kwake kando
kando ya barabara na bado kuna watu wanakuwa wanamfuatilia na kumwambia kwamba
anatakiwa kuichangia serikali kwa njia ya ushuru. Mama huyu ameishi kwa
biashara hii kwa muda mrefu kwani inaonekana hata wakati Kikwete ameingia
madarakani na kutangaza kutoa mabilioni yaliyoitwa mabilioni ya Kikwete kwa
wafanyabiashara wa hali ya chini alikuwapo na biashara yake. Aliambiwa
atapatiwa mkopo na kimsingi ofisi ya mtaa iliwachangisha shilingi elfu 50 kila
mmoja ili wapate hiyo mikopo ya mabilioni ya Kikwete. Lakini anasema hadi leo
tunapoongea hawajaiona hiyo mikopo. Mwendesha kipindi alikatisha ghafla na
kuwauliza washiriki wake, ni nani aliyewahi kupata huo mkopo, hakuwepo ukumbi
mzima. Ni nani anamjua mtu aliyepata huo mkopo, ni kijana mmoja tu ndiye
aliyekiri kwamba rafiki yake mmoja aliupata. Mwendesha kipindi akauliza tena ni
nani sasa waliopata hiyo mikopo. Watu walibaki kimya. Na wakati mama Editha
anaendelea kuyaelezea maisha yake, mpiga kamera alielekeza kamera yake kwa
umati uliokuwa ukumbini ukimsikiliza. Nilitazama haraka haraka nyuso za watu
wale nikaona zilivyojaa huzuni na wengine wakitikisa vichwa.
Mimi niliyekuwa nafuatilia kutoka nyumbani kwangu nikiwa
nimekaa kwenye kochi kadiri nilivyomsikiliza yule mama niliwaza mbali sana na
kwa kweli wakati mpiga picha akiwaonesha waliokuwa ndani ya ukumbi wakitikisa
vichwa, mimi machozi yalikuwa yakitoka. Niliwakumbuka kina afande Hiza na
Nicholaus na juhudi zao za kuhakikisha mimi naenda gerezani Keko. Picha zao
ziliniijia mawazoni tena na kuwatazama jinsi walivyobebelea matumbo makubwa
yaitwayo vitambi.
Nikakumbuka magari yao
mazuri ya kazini na ya kwao binafsi. Nikajiuliza kama wanaelewa wanachokifanya
na kama mimi wanayenikamata kwa kuwapigania
hawa kina mama Editha wananifahamu vizuri.
Nilijiuliza kama wanafahamu vema maisha ambayo nimeyapitia.
Hivi wanajua kwamba katika Kitongoji cha Nansuruli, Kijiji cha Nakatuba, Kata
ya Kibara, katika Jimbo la Mwibara wilayani Bunda, Mkoa wa Mara ambapo ndipo
nilipokulia umbali baina ya kitongoji na kijiji ni kama
kilometa 20. Na huko ndiko tulilazimika kupata huduma zote muhimu, ikiwa ni
pamoja na shule, gulio la pamba (zao letu la biashara), soko (la samaki tu) na
usafiri (wa msimu). Ili tuwahi shule saa 12:30 asubuhi, ilitulazimu tuondoke
nyumbani saa 11 alfajiri. Tulichapa mguu hadi shuleni, hapakuwa hata na
baiskeli na kwa upande wa gari, si tu kwamba halikuwepo bali hapakuwa hata na
njia ya kulipitisha. Tulisoma hadi saa 6:10 mchana na wenzetu walienda nyumbani
kwa chakula cha mchana hadi saa 8 mchana.
Sisi tulilazimika kukaa shuleni bila kwenda kula kwa sababu
tunatoka mbali. Hata hivyo wenzetu waliporudi tuliendelea na vipindi kama kawaida hadi saa 9:30 mchana tulipoanza wakati wa
kazi. Wakati wa kazi ulikuwa ni kwa ajili ya kazi kama
kulima au kupalilia mashamba ya walimu waliyojigawia kuzunguka shule.
Wengine walifanya kazi nyingine kama kufyeka, kupanda au
kumwagilia maua, kupanga mawe, kuzungushia uzio kwenye nyumba za walimu, na
wengine hasa wasichana walikwenda kufanya kazi za nyumbani kwenye nyumba za
walimu kama vile kuosha vyombo, kudeki, kuchota maji, n.k. Tulioshinda njaa
hatukupewa upendeleo, tulishiriki kazi zote hizo kama wenzetu waliokuwa
wamekula.
Tulitawanyika saa 10:30 jioni na tukafika nyumbani saa 12
jioni. Tulikuta wazazi wakiwa wametuwekea ugali wa mhogo uliopikwa mchana.
Ulikuwa umepoa na kuwa kiporo kigumu.
Baada ya kula tulikwenda kufuatilia mifugo kutoka machungani
na kuwarejesha nyumbani na kufanya kazi kama kukamua maziwa, kuandaa moto wa
kuota usiku na wazee wakati tukisubiri chakula cha usiku. Wasichana waliporudi
kutoka shule walikabiliwa na kazi kama kuchota maji, kuokota kuni na kuandaa
chakula cha usiku. Muda wa kulala ulipowadia tulitafuta ngozi za ng’ombe ambazo
ndizo zilikuwa vitanda. Ngozi ambazo mchana zilitumika kwa shughuli nyingine
kama kukausha nafaka, usiku tulizikung’uta mavumbi na kuzitandika chini na
kulalia, tena wakati mwingine bila shuka la kutandika, na la kujifunika likiwa
limechanika chanika.
Shuka lililonunuliwa likiwa jeupe ilifika mahali huwezi
kutambua rangi yake maana hatukufua kwa sabuni bali mara nyingi tuliponda ponda
majani ya mipapai na kutengeneza povu kidogo na kulitumia hilo kufua. Hatukuwa na viatu. Katika shule
ya wanafunzi 400 ungeweza kukuta ni wanafunzi wasiozidi 10 waliokuwa na viatu, wengi
wao wakiwa ni watoto wa walimu na wazazi wachache wenye uwezo kijijini.
Tulitembea umbali wote wa kutoka nyumbani hadi shule bila viatu. Tulitembea
madarasani na nje ya madarasa bila viatu, tuliingia chooni bila viatu na
tulitembea sehemu zenye miiba na zisizo na miiba, bila viatu.
Siku za wikendi zilikuwa ni siku za kutafuta pesa kidogo kwa
ajili ya mahitaji ya lazima kama kununua
penseli/kalamu, chumvi (ile ya mabongemabonge), mafuata ya dizeli (siyo ya
taa), n.k. Pesa hiyo tuliipata kwa kubeba mizigo ya kuni kwenda kuuza mjini
umbali wa zaidi ya kilometa 20. Nakumbuka mimi nilikuwa nikiuza mzigo wangu kwa
sh 10 na dada na shangazi wao waliuza sh 30 kila mmoja. Mizigo ya kuni ya
watoto watatu au wanne wakati mwingine, yote ilibebwa kwenye kichwa kimoja tu
cha mama yangu kutoka mlimani na kuleta nyumbani.
Baadaye mama yangu amekuja kusumbuliwa sana na kifua na hatimaye akapata stroke
ambayo imemwacha akiwa amepooza upande mmoja. Madaktari wamethibitisha kwamba
kifua kiliharibiwa na mizigo mizito aliyokuwa akiibeba zamani.
Kule nyumbani Hospitali iliyoko karibu zaidi na kwetu ni ya
mission ambayo iko umbali wa kilometa kama 25
hivi kutoka nyumbani.
Mama yangu alipoumwa uchungu wa mtoto wa sita alisindikizwa
kwa mguu kwenda hospitali. Kwa sababu ya kutembea na uchungu ukiwa umeanza,
alizidiwa na kukimbilia kwenye kichaka kilichokuwa karibu na njia na
akajifungua mtoto wa kike akiwa nusu ya safari ya kutoka nyumbani kwenda
hospitali.
Haya ni mambo machache niliyopata kuyaelezea huko nyuma
kuhusu maisha yangu ya utotoni. Nimeyarudia kwa sababu najua kina Dk. Lupembe
wakati huo hawakuwahi kuyasoma. Lakini nimeyarudia ili ofisi ya DCI
inayofuatilia sana
makala zangu kwa sasa ijue nilikotoka na niliko na sababu ya kuwa kwangu huko.
Kwa taabu kubwa namna hiyo nilifanikiwa kusoma mpaka nikaja
kupata elimu ya chuo kikuu. Naomba niseme hapa hadi mwezi Machi mwaka huu ‘pay
slip’ yangu inaonyesha kwamba mshahara wangu ulikuwa sh milioni moja na laki
sita kabla ya makato nikiwa mtumishi wa Umoja wa Mataifa kwenye Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda
mjini Arusha.
Huo ni mshahara ambao nina uhakika Afande Hiza na Mwenzake
Nicolaus hawajapata ndoto ya kuwa nao. Ningeweza kutulia na mshahara huo ambao
ulishaniwezesha kununua gari, kiwanja kikubwa na nilishaanza kujenga, watoto
wanasoma shule za English medium, nyumbani nawasaidia wazazi kila mwezi ikiwa
ni pamoja na kuwasaidia kuongeza na kuitengeneza vizuri nyumba yao, nasomesha
wadogo zangu, nasaidia wazazi wa mke wangu na kadhalika.
Lakini wengine waliotapakaa kwenye kila kona ya vijiji na
mitaa ya Tanzania
hii wanaendelea na maisha pengine magumu zaidi ya yale niliyoyaishi mimi
utotoni. Watoto wa Mama Editha hawajafanikiwa na pengine hawatafikia
nilipofikia mimi. Na sasa kila anayebahatika kufika nilipofika mimi anatulia na
kutengeneza maisha yake na ya wazazi wake, ni nani atawapigania mamilioni ya
waliobaki?
Ninapofika hapo na nikikumbuka kwamba baba yangu kanilipia
ada mwisho kidato cha nne bali nilipokuwa DIT nilijilipia kutokana na fedha ya
mafunzo viwandani na chuo kikuu nikapata mkopo, ndipo najikuta kwamba nadaiwa
na Watanzania wote. Nimetumia kodi ya Watanzania wote ili nipate ufahamu
nilionao na ni makosa kuwaacha.
Nikaandika barua ya kuacha kazi pale Umoja wa Mataifa ambako
walianza kuniambia niache siasa. Nikabaki kuwapigania Watanzania nikiwa ndani
ya CHADEMA nikishiriki kutafuta mabadiliko. DCI Manumba na wapelelezi wake
hawakujua nilikotoka. Wakadhani wakinikamata na kunipeleka Keko
wataninyamazisha.
Ni bahati nzuri sana
kwangu kufika kule maana nimegundua kuna Watanzania wengine lukuki kule ambao
wanahitaji kupiganiwa.
Wale vijana walioachishwa kufanya shughuli zao kwa tamaa ya
vijana wa DCI ambao wamechoka kufanya kazi wanachotaka ni kuchumia matumbo tu.
Kwamba mtu anakufa leo kesho askari wa upelelezi anauliza hiyo kesi ya mauaji
imepata mtu?
Akijibiwa bado anasema mpe huyu! Na huyu akitoa pesa hana
kesi, anaachiwa mara moja na kutafutwa mwingine wa kupewa. Ukitaka kuwajua
angalia kesi yangu. Nimekaa chumbani kwangu nimeandika makala bila
kumshirikisha mtu yeyote, nimeituma kwa mhariri naye kaipitisha jinsi ilivyo
baada ya kuipitia na hatimaye inatoka kwenye gazeti.
Wakubwa wanaisoma hawakuipenda. Wapelelezi wanakabidhiwa
kuhakikisha huyu ‘mchochezi’ analala Keko. Wananikamata na kunihoji na gazeti
wanalo ofisini kwao. Lakini mpaka leo wanadai upelelezi haujakamilika.
Wanapeleleza wapi?
Vijana mlioko magerezani nchi nzima kwa kuonewa, ukombozi
wenu umekaribia. Endeleeni kuvuta subira miaka michache sana
iliyosalia hamtaamini kwamba Tanzania
mtakayokuwa mnaishuhudia ndiyo ile mliyoishi miaka yote hii.
Hamtaamini kwamba Wambura anayewatesa ndiye yule mtakayekuwa
mnamwona wakati huo. Kina Nicolaus na wanaotamba leo lazima Mwigamba alale
ndani hawataamini macho na masikio yao.
Yatunzeni maandishi haya na mawasiliano yangu mtaniuliza miaka michache sana ijayo kwamba wakati
naandika nilikuwa naona nini mbele! Kwa ajili yenu kina mama Editha nimejitoa
kwa kila kitu kuwapigania na kama ni kunikamata kwa ajili hiyo watanikamata sana!
CONGO
CONFLICT
Congo conflict is a long and a crisis which is
highly experienced in the eastern part of the democratic republic of Congo
(DRC) and it is regarded by the western countries as the African First World
War.
v
Congo gained its
independence in 1960 and became under Patrice Lumumba who was overthrowened by
Mobutu Se Seseko in 1964
v
In October 1996, Rwanda
troops (RPA) entered DRC with an army coalition led by LAURENT DESIRE KABILA
known as AFDL and in 17th may 1997 Kabila declared himself a president;
he was also supported by Uganda.
v
In 2000 Kabila was gunned down and replaced by his son
JOSEPH KABILA at the age of 31.
v
Congo is the 3rd
vastness country in Africa
v
Congo has almost 200 ethnic groups speaking different
languages, but the most large groups are
·
Luba
·
Kongo
·
Anamongo
v
Congolese Tutsi as well as the government of Burundi, Rwanda
and Uganda, all relied on the Rwanda
military presence in DRC for the protection against hostile army groups
operating from the eastern part of the country.
·
The Interahamwe militia of the HUTU ethnic, mostly from Rwanda which fought TUTSI- dominated government
of Rwanda.
·
HUTU members of the former Rwanda armed forces
·
Mayi mayi, a loose association of traditional Congolese
local defense forces which fought the influx of Rwanda immigrants.
·
The Alliance of Democratic
Forces (ADF) made up of Uganda
expatriates and supported by the government of Sudan.
·
Several groups of HUTU from Burundi
fighting the TUTSI dominated government of Burundi.
TYPE OF THE
CONFLICT
Congo conflict is the
state control/failed state.
PARTIES INVOLVED IN THE CONGO CONFLICT
v
The government of the Democratic Republic of Congo
led by JOSEPH KABILA
v
Several armed groups (Congolese Rally for Democracy –RDC,
Kisangai/Movement de Liberation).
v
Rebels movement
·
Movement for Liberation of Congo
(MLC) under PIERRE
BEMBA
·
Mayi mayi militia fighters under KYUNGU MUTAGA
·
The National Congress for Defense of Congolese People (CNDP)
faction in the northern kivu
v
Foreign rebels.
·
Burundi forces; Forces
for Defense of Democracy (FDD)
·
Forces Democratique de Liberation (FNZ)
·
Rasta Movement, former Hutu militants
·
Lord’s Resistance Army (LRA)
v
International forces involved in peace support operation
·
MONUC – UN mission in the DRC since 1999
·
German led European Union Mission.
·
CAUSES OF THE CONFLICT
v
Struggle for political power, USA backed MOBUTU to overthrow
LUMUMBA in 1990’s - Antonio Gezanga
declared himself a Prime Minister
v
Bad governance (Dictatorial) – Mobutu in 1965 led to the
civilian revolt
v
Conflicts over basic resources such as water
v
Access and control over rich minerals areas and their
resources, cobalt, diamond, copper….Moise Tshombe declared Katanga a free province from Congo
v
Nepotism
v
Regionalism…Bas Congo, Kasai etc
v
Rebels movements…..refugees from Rwanda
and Burundi
v
Ethnicity….Bagaulla group was very strong
v
Assassination of leaders
IMPACTS
v
Death of people…..from august 1998 to April 2004, 3.8
million death were reported
v
Starvation and diseases
v
Refugees
v
Human rights violations.
WAYS TOWARDS PEACE
v
1998 an agreement was signed (LUSAKA
PEACE AGREEMENT) by key rebel movement (NLC), Congolese Liberation Movement
Rary for Congolese Democracy (RDC) with government of Kinshasa.
v
Democratization….2006,first general election in 40 years
then 2011
v
Peace keeping operation.
v
MONUC...since 1999, since 2005 it has stepped up active
military actions
v
EU mission led by German
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA UMMA.
31/10/2011.
JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA
DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu. Sina wakati m...gumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.
Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee
wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.
Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.
Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema.
MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE, MUNGU YUPO UPANDE WETU.
Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.
Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu. Sina wakati m...gumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.
Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee
wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.
Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.
Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema.
MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE, MUNGU YUPO UPANDE WETU.
Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.