FOLLOWERS

Friday, July 20, 2012

SIMULIZI : WAZIRI WA MAMBO YOTE SEHEMU YA 2

Na Fredy Julius

WAZIRI WA MAMBO YOTE SEHEMU YA 02

ILIPOISHIA                                                                          
Chriss hapo hata mimi naona kama mbunge sio wetu bali ni wa chama ambacho ndio kimempa madaraka na kina uwezo wa kumnyang’anya madaraka hayo, hapo kwa vyovyote ni lazima mbunge awajibike kwa chama chake, hiyo iko wazi. Sasa umeona? Achana na huyu wa jimbo letu, je hawa wa kuteuliwa watawajibika kwa nani ikiwa hawachaguliwi na wananchi? Kwa vyovyote vile ni lazima watawajibika kwa chama chao na ndiuo maana utawaona wabunge wa kuteuliwa wa chama tawala wanashabikia sera na mipango amabayo haina mantiki wa tija kwa maendeleo ya taifa hili hata kidogo, maswali ya msingi nay a nyongeza wanayoyauliza hayaeleweki na wanaongoza kwa kuwasifia mawaziri, utasikia “ namshukuru sana muheshimiwa waziri kwa majibu mazuri na yenye kuleta tija, na kwa kuwa naamini serikali ya chama changu ni sikivu basi naamini haya yatatendewa kazi, lakini hata hivy muheshimiwa spika nina swali dogo moja la nyongeza, kwa kuwa ni tangu mwaka juzi serikali imewaahidi wanachi wa mkoa wangu kuwa misaada na mikopo kwa akina mama na wajasiliamali wadogowadogo itafikishwa moja kwa moja kwa wahusika, na kwa kuwa wahusika wanalalamika kila siku kuwa mpaka leo hawajapata hayo mabilioni tangu yalipotolewa, sasa je, ni lini mheshimiwa wazri atawawajibisha watendaji wake na kuwaagiza kuwa wahakikishe wanapeleka pesa hizo moja kwa moja kwa wananchi badala ya kupitishia katika mtirirIko huo ambao unasababisha ubabaishaji mwingi na hatimaye wanachi wengi wa hali ya chini kuzikosa pesa hizo”?. Sasa hapa utajiuliza uhalali wa kusifia majibu yaliyotolewa na waziri pamoja na kuuliza swali la nyongeza kama hilo……………….SASA ENDELEA
            Naona tumefikia wakati muafaka, ndio mchangiaji wa kwanza anataka aanze kuchangia ule muswaada wa mabadiliko ya sheria ya manunuzi yetu, labda hawa jamaa wanaweza kuamua wasiipitishe hii sheria maana inavyoonekana haina mashiko. Aah wapi, kama wabunge wa chama tawala wameshaafikiana itapita tu, poa ngoja tumsikilize mchangiaji wa kwanza ndio anaanza. “ mheshimiwa spika nakushuru kwa kunipa furs hi ya kuwa mchangiajai wa kwanza  katika muda wa jioni, mimi naomba nijielekeze katika kipengele huki cha tatu ambacho kunairushusu serikali kununua…….,aaaaahhhhhhhhhhh TANESCO. Duh jamaa wameshatuharibia, yaani kulikuwa kumetulia ni kama hawatakata hivi. Duh Chriss, hivi hata hawa majirani zetu nao wana mgao wa umeme kwa kiwango hiki sababu tu ya upungufu wa maji? Sidhani kama jamaa wana mgao mkali kama huu kwa sabau tayari hawa jamaa wa wizara husika wanafanya mazungumzo na moja ya makampuni kutoka kwa hao hao majirani zetu ili wawauzie sijui wawakodishie majaenereta kwa ajili ya kufua huo umeme wa dharula, sasa kama kwao hautoshelezi wanawezaje kutukodihia sisi?. Aah isije ikawa yale yale ya kutengeneza mvua ya kisasa kwenye bwawa la mtera malakukodisha mitambo ya kufua umeme wa dharula mala waapi hakuna umeme wala nini. Sijui kaka ila kikubwa ni kwamba tusubiri tuone itakuwaje.
Sasa Ephraim tunafanya nini, maana huu umeme kurudi ndiyo hivyo tene mpaka usikuu. Kama vipi tukaangalie mechi uwanjani maana ligi darajaa la pili sijui la tatu ngazi ya mkoa imeshaanza na leo kuna mechi. Wanacheza timu gain na timu gain?. Nasikia ni timu ya kurugenzi na timu gain sijui kutoka njombe. Basi poa tujibebe bebe telekee uwanjani tukaangalie mechi maana hapa hapana ladha tena, japokuwa mpira wa hapa kwetu umeshapoteza umaarufu sana tofauti na enzi zile tunasoma shule ya msingi,mtu unakuwa radhi kesho ukachapwe bakora na mwalimu mkuu kwa kutokurudia shule lakini siyo kuikosa mechi ya Sawala FC ya mufindi na Streto kutoka iringa mjini ilikuwa inakuwa patashika na burudani ya kutosha sana. Halafu cha kushangaza tangu enzi hizo sijawahi kusikia wachezaji kutoka wilaya za huku kwetu wakicheza ligi kuu zaidi ya kina Haji Mbelwa na Titho Andrew basi bwana. Soka letu bado linahitaji nguvu nyingi sana ili kulirudisha pale lilipokuwa zamani chriss.
Hivi Ephraim unataka kuniambia kuwa mpira wa Tanzania hii unaweza kurudisha hadhi ile ya zamani kweli? Kunhijtajika uzalendo na jitihada kubwa sanaa kurudi kule tulikokuwa tumefika kimpira, enzi hizoo sijaanza hata shule ya msingi nakumbuka tu na ka redio ka mkulima, mzee na mjomba walikuwa hapitwi na mechi na ikawa ndio mwanzo wa mimi kuwafahamu wachezaji wakubwa na mahiri wa nyakati zile. Wachezaji kama Bakari Malima “ jembe ulaya”. Thomasi Kipese, Edward Chumila,Said Mwamba Kizota, sikumbuki vizuri walikuwa wancheza timu zipi kwani nilikuwa baado kinda na wala nilikuwa sijajikita katika kuufuatlia mpira kwa kiwango kikubwa, ila baada ya kukuka ndio nikajua, zilipokukja nyakati za akina Mohamed Hussein “ mmachinga” Edibil Jonas Lunyamila, Rajabu Mwinyi, Salvatory Edward, akina Nteze John “ lungu”, Mohamed Mwameja akina Peter Manyika na wengine weengi ilikuwa inakuwa patashika samba na yanga, enzi hizo timu kama Reli ya Kigoma na Tukuyu Stars zilikuwa ziko vizuri sana na zinatoa changamoto kwa watani wa jadi tofauti na ilivo siku hizi kaka. Kweli, lakini kama viongozi na wachezaji wataamua na kujua ni nini wanatakiwa kufanya ni lazima mpira wetu utarudisha hadhi ile ya zamani na sisi angalau tukashiriki kwenye michuano mikubwa ya bara na hata siku moja kombe la dunia. Kweli ila kuna kitu kimoja kikubwa ambacho viongozi na wadau wanatakiwa wakifanyie kazi kwa nguvu.
Kuwekeza katika soka la vijana ni suala lamsingi sana na ni lazima kila moja afanye kazi kwa moyo wa uzalendo katika nafasi yake vinginevyo tutakuwa tunashabikia na kushangilia timu za mataifa ya afrika magharibi kila siku na kuishia kushabikia ligi za wenzetu wa ulaya ijapokuwa hatujifunzi kitu chochote ni kwanini wenzetu wanfanikiwa na sisi bado tupo paleplae kila mwaka na la zaidi ni kwamba tunarudi nyuma. Mimi nakumbuka tulikuwa na mwanafunzi mwenzetu ambaye nimesoma naye darasa moja anaitwa Agano, alikuwa fundi kweli kweli wa mpira,yaani alikuwa anaucheza ipasavyo mpaka akaingia katika matatizo na mkuu wa shule kuhusu msichana mmoja alikuwa anaitwa Winnie. Agano alikuwa maarufu kwa jina la namba tisa kutokana na kucheza na kuimudu vema nafasi ya ushambuliaji na hivyo wanafunzi wote tukamzoea kwa jina hilo,ijapokuwa kwa sisi tuliokuwa karibu naye tulijua na siri nyingine ya kuitwa jina hilo la namba tisa amabayo wengine hawakuijua zaidi ya kujua kuwa ni kutoka na yeye kucheza katika nafasi ya ushambuliaji na kuwa anafunga sana magoli basi. Lakini nyuma ya pazia agano alikuwa ni mtu anayependa sana wasichana, namba tisa ilisimama kwa idadi ya wasichana tisa ambao alikuwa akiwamiliki. Japokuwa mkuu wa shule alimpenda sana kutokana na kuwa alikuwa anaipa sifa nzuri kimichezo ilimbidi amfukuze shule sit u kwa kuwa alikuwa amefanya makosa bali ni kwa kisasi  na chuki baada ya kugundua kuwa mkuu wa shule na agano walikuwa wanachangia msichana mmoja kati ya wale tisa ambao agano alikuwa anawamiliki.
            Huyu ni binti  Winnie, aliyekuwa kidato cha sita kwa wakati huo,pasipo kujua kuwa kumbe mkuu wa shule naye alikuwa anajihudumia hapo kwa siri kubwa, agano alijikuta akiiingia katika mahusiano na Winnie kutokanan na shinikizo lake Winnie mwenyewe kwa agano,na kawaida ya agano ni kumuacha msichana mmoja kila alipopata msichana mwingine mpya, safari hii ilikuwa ni zamu ya Christina kutengenezewa hila na kuachwa ili nafasi yake ichukuliwa na Winnie na hivyo kuendelea kuwa na namba ilie ile tisa katika idadi yake. Baada ya kuachwa Tina hakuwa na la kufanya, lawama nyingine kwa mpenzi wake huyo lakini ilikuwa ni sawa na kazi bure kwa yeye hakujali hata kidogo. Mapenzi na Winnie yakanoga kiasi ikafikia wasichana wake wengine wakajikuta wanagundua kuwa kila mmoja kwa nafasi yake alikuwa akiongopewa kuwa yuko peke na kutokana na kuelewa na sifa alizokuwa nazo agano hapo shuleni wakajikua wakianguka katika mtego wake na kuchezewa kwa nyakati tofauti bila wao kujitambua. Tafrani iliyoibuka baada ya mabinti hawa kuushtukia mchezo wa mpenzi wao ndio iliyopelekea agano na wiinie kufukuzwa shule kutokana tu hasira na kisasi cha mkuu wa shule kwa wote wawili huku hawa wengine nane wakipona na kupewa onyo kali.
            Mapenzi ya siri kati ya mkuu wa shule na mwanafunzi wake huyo yalianza kwa siri sana kupitia makosa ambayo Winnie aliyafanya na mkuu wa shule kuamua kutumia nafasi hiyo kutimiza  haja na tama zake za kimwili juu ya binti huyo. Ndani ya gari akiwa katika safari yake ya kikazi kuelekea katika mkutanoo mkuu wa chama cha wakuu wa shule Tanzania ambao ulikuwa unafanyika katika makao makuu ya mko mkuu wa shule anakutana na mwanafunzi wake na katika kumtazama tu akajua akuwa lazima amendoka shuleni bila kupewa ruhusa kutokana na hamaki na mshangao alioutoa baada ya kumuona mkuu wa shule ndani ya gari. Kwa kuwa walikuwa wanashuka kituo kimoja ikabidi mkuu wa shule amuite na kumuuliza ni wapi alikuw anakwenda na amepewa ruhusa na nani kusafiri nje ya shule?. Winnie hakuwa na jibu la kumpa mkuu wa shule akaridhika na kujikuta akiishia kumuomba msamaha kwa kosa hilo.
            Kwa kuamini kuwa yuko mbali na shule kwa muda huo na hakuna ambaye angejua kirahisi ni nini amefanya huko aliko mkuu wa shule akaamua kumuweka sawa mwanafunzi wake..unaenda wapi ikiwa sasa ni jioni?..mwalimu mimi naenda kwa rafiki yangu kumsalimia nilipata taarifa kuwa anaumwa sana..nyumbani kwenu baba ba mama yako wanatambua kuwa wewe hauko shule muda huu?..hapana hawajui sijwataarifu..na ni kwanini hujawataarifu?..sikupenda tu wajue kuwa nimekuja huku kumsalimia rafiki yangu. Sasa sikiliza, tunaongozana na mimi kuelekea mahali nilipofikia ili tukazungumze vizuri ni kwanini hujaomba ruhusa na ni kwanini umekuja huku bila wazazi wako kujua, utakaponipa maelezo ya kueleweka ndipo nitakapo kupa ruhusa ya kwenda kumsalimia huyo rafiki yako vinginevyo utarudi shule muda huu huu na utajua wewe ni vipi utapata usafiri wa kukurudisha huko.
            Majadiliano kati ya mkuu wa shule na mwanafunzi wake yalifanyika ndani ya chumba cha kulala wageni katika hoteli ambayo mkuu wa shule alikwa amefikia hapo mjini. Ukali na misimamo katika maamuzi ni vitu ambavyo huathiriwa na mazingira na watu ambao mtu unakuwa nao katika wakati hu. Winnie akajikuta anakosa maneno ya kusema na neon lake likawa nisamehe. Kwa kila swali ambalo mkuu wa shule alimuuliza jibu lake likawa naomba unisamehe mwalimu. Ndipo mkuu wa shule alipojiridhisha kuwa sasa anaweza kumwambia lolote na akamtii. Sasa sikiliza binti, mimi hapa nimekuja peke yangu leo huku, utalala na mimi kwa leo kwa leo halafu kesho utaenda kumsalimia huyo rafiki yako na keshokutwa baada ya kikao kumalizika utakuja hapa tutalala wote ili asubuhi tuondoke pamoja kurudi shule sawa?. Sawa mwalimu nimekuelewa.alijua wazi kuwa kumkatalia mkuu wa shule kulimaanisha kuwa kufukuzwa shule kwa sababu ni kweli alikuwa amevunja sheria za shule.
            Akiwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo zilizomuwezesha kuishi mjini bila kuwa na wasiwasi wa kukosa chochote, amepanga nyumba nzima na anamiliki gari la kutembelea, ilikuwa ni kazi rahisi sana kwa kijana Aidani kumpata msichana yeyote yule aliyemtaka na kwa wakati wowote kutokana na tama za wasichana wengi wa mjini. Kutosikia lolote kutoka kwa Winnie mpaka kufikia muda huo wa usiku na simu yake kuwa imezimwa kulimtia wasiwasi Aidani ila alishindwa kujua kuwa ni nini kimempata mpenzi wake kwani mpaka anakaribia kufika mjini walikuw wanawasiliana nay eye kuingia barabarani kwenda kumpokea lakini alipofika kituo cha mabasi hakumkuta na alipojaribu kupiga simu yake ilikuwa haipatikani. Akajipa subira kuwa huenda akawa amekwenda nyumbani kwao na hivyo atamtafuta kesho licha ya kuwa alimwambia anakuja kwake na nyumbani kwao hawajui lolote kuhusu safari hiyo ya yeye kwenda mjini……………….ITAENDELEA

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...