Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Ijumaa Octoba 14 ya kila mwaka watanzania wote kote duniani huungana pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa taifa hili hayati Julius Nyerere. Ni siku ambayo hutukumbusha majonzi tele yasiotarajiwa kuja kukauka kamwe...ni siku ambayo baba wa taifa aliaga dunia katika hospital ya Mtakatifu Thomas huko London Uingereza
kumbukumbu hizi huambatana na shughulu mbalimbali zenye lengo la kuenzi fikra, wosia na falsafa za baba wa taifa. Binafsi ningependa kuwasisitiza watanzania wenzangu tuenzi na kudumisha falsafa za baba wa taifa kwa kusisitiza utawala bora wenye kufuata misingi ya haki, utawala bora na katiba japokuwa kuna mapungufu lukuki katika katiba tuliyonayo kiasi cha kulia kila iitwayo leo kufanywa haraka kwa mchakato wa kuandika katiba mpya yenye manufaa na maslahi kwa watanzania walio wengi.
Mwalimu Nyerere alilinda na kuiheshimu katiba kiasi cha kila mtanzania kuridhika na utawala wake, ni katiba hii hii yenye mapungufu lukuki ambayo baba wa taifa aliiheshimu na kuilinda kiasi cha watanzania kukubali utawala wake. hakuhubiri udini hata kidogo kwa sababu alijua ni kinyume na katiba, alisisitiza haki, usawa na haki baina ya raia wote wa Tanzania.
Ni jinsi gani viongozi wetu wa leo wanaongozwa na katiba na sheria ndilo swali kubwa tunalopaswa kujiuliza na kutafuta majibu........kwa mfano, katiba inatamka wazi katika ibara ya 3 (1) kuwa "jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.". je kuna uhalisia katika mifumo ya kututawala iliyojengwa na viongozi wetu wa sasa ya kuwa kuna demokrasia?..je si ni hawa hawa baadhi ya watawala wetu wanaoamua kutugawa kwa misingi ya udini?
Vile vile katiba inatamka wazi katika ibara ya 13 ibara ndogo ya 6, kifungu (a) ".kwa
madhumuni ya kuhakikisha haki na usawa mbele ya sheria, mamlaka ya nchi
itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia msingi kwamba;...wakati
haki na wajibu kwa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na
mahakama au chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa
na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya
kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi
ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika.". Je ni watanzania wangapi ambao bado haki na usawa mbele ya vyombo vya sheria ni ndoto kwao??
No comments:
Post a Comment