FOLLOWERS

Sunday, September 16, 2012

HADITHI :WAZIRI WA MAMBO YOTE SEHEMU YA TATU

Na Fredy Julius

WAZIRI WA MAMBO YOTE SEHEMU YA 03

ILIPOISHIA  
Akiwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo zilizomuwezesha kuishi mjini bila kuwa na wasiwasi wa kukosa chochote, amepanga nyumba nzima na anamiliki gari la kutembelea, ilikuwa ni kazi rahisi sana kwa kijana Aidani kumpata msichana yeyote yule aliyemtaka na kwa wakati wowote kutokana na tama za wasichana wengi wa mjini. Kutosikia lolote kutoka kwa Winnie mpaka kufikia muda huo wa usiku na simu yake kuwa imezimwa kulimtia wasiwasi Aidani ila alishindwa kujua kuwa ni nini kimempata mpenzi wake kwani mpaka anakaribia kufika mjini walikuw wanawasiliana nay eye kuingia barabarani kwenda kumpokea lakini alipofika kituo cha mabasi hakumkuta na alipojaribu kupiga simu yake ilikuwa haipatikani. Akajipa subira kuwa huenda akawa amekwenda nyumbani kwao na hivyo atamtafuta kesho licha ya kuwa alimwambia anakuja kwake na nyumbani kwao hawajui lolote kuhusu safari hiyo ya yeye kwenda mjini………SASA ENDELEA

Usiku ule ulikuwa ni mtamu zaidi kwa mkuu wa shule, licha kuwa alimpata Winnie kirahisi tofauti na alivyokuwa akifikiria kutokana na msimamo aliokuwa akiounesha kwa wavulana na hata baadhi ya wanafunzi wenzie pale shuleni, hakuwa na fikra za kuwa na mwanamke katika usiku huo hivyo akaona kwamba safari yake imekuwa ya neema. Kwa woga na aibu Winnie alimpa penzi mkuu wake wa shule usiku ule huku akilini mwake akiwa na wazo moja tu, atamwambia nini Aidani kesho yake asubuhi. Raha na utamu kutoka kwa mwanafunzi wake vilimfanya mkuu wa shule asitamani usiku ule uishe ili aendelee kumfaidi mwanafunzi wake yule. Baada ya kama masaa matano ya kupeana raha wakapata usingizi huku wote wawili wakiwa wamechoka taabani.
            Kikao kilipangwa kuanza saa mbili kamili asubuhi, na kwa raha na mchaka mchaka alioupata kutoka kwa mwanafunzi wake mkuu wa shule alijikuwa akishtuka saa tatu na nusu asubuhi. Ilimbiid ajiandae haraka haraka na akaachana na Winnie akielekea kumsalimia rafiki yake huku akimpa kiasi kadhaa cha pesa na kumsisitizia kuwa kesho arejee tena ili walale wote na hatimaye keshokutwa waondoke pamoja kuelekea shuleni. Winnie akshika njia mpaka katika kituo cha taxi akakodi na kuondoka huku akiwassha simu haraka haraka na kumtafuta Aidani, simu ilikuwa ikiita bila kupokelewa, akapiga tene na tena na tena lakini haupata majibu yeyote. Aliendela kupiga simu mpaka gari inafika nyumbani kwa Aidani simu ilikuwa bado haijapokelewa. Akamlipa dereva nay eye akashuka na kueleka mlangoni. Akapiga hodi!!.
            Aidani kwa kuwa alijua fika kuwa Winnie amekuja ila bila kujua kama ni makusudi au imetokea bahati mbaya wakashindwa kuonana alimua ijumaa hiyo akale raha disko baada ya kunywa pombe na kulewa chakari akajikuta katika matatizo baada ya kugombana na kijana mwingine ambaye yeye hakumjua kumbe alikuwa ni motto wa tajiri na kigogo wa serikalini. Katika purukushani na fujo zile kijana yule alijigonga ukutani akandoka na kupoteza fahamu. Walinzi wa ukumbi waliokuwapo mahali pale wakamkamata Aidani na kasha kutoa taarifa polisi ambapo baada ya taratibu zote kijna yule akafikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu na Aidani akachuliwa na polisi na kuswekwa sero.
            Asubuhi na mapema baada ya kuamka akiwa amesurubiwa vizuri na baridi na mbu wa mle ndani kiasi kwamba hakuweza kulala vizuri akaomba msaada wa simu yake ili aweze kuwataarifu ndugu zake kuwa yeye yupo mikononi mwa polisi. Kutokana na kuhofia ni nini ambacho baba yake angemjibu akaamua kumpigia rafiki yake wa karibu Sunday, baada ya kumueleza kila kitu kilichotokea ikabidi Sunday aelekee kituo cha polisi ili kwenda kumuonan rafiki. Akapewa ruhusa ya kuzungumza naye
“……...aidani vipi tena mbona huku ghafla bila hata taarifa?,,
“……….aahhaa kaka jana disko bwana nimelewa kukatokea fujo nikapigana na jamaa mmoja hivi ndiyo ikawa yote haya..
“…..sasa unafikiri inakuwaje hapa?
“..hapa kikubwa kwanza fuatilia habari ya dhamana halafu mambo mengine tutajua nikiwa nje.
“……………..Sasa dhamana si ni mpaka ufikishwe mahakamani?..ndiyo muda sio mrefu wamedai watanipeleka mahakamani kwa hiyo iyabidi uje huko ila saa hizi chukua funguo za nyumbani hizi ukaniletee angalau nguo za kubadilisha kaka.
            Baada ya kugonga mlango kwa muda mrefu bila majibu ndipo Winnie alipoamua kuchukua kiti kilichokuwa pale nje na kukaa ili amngoje Aidani na ajue ni nini kimempata maana simu yake bado ilikuwa inaita bila kujibiwa. Baada ya muda kama wa nusu saa hivi akaona gari inakuja na ikapaki usawa wa mlango wakashuka watu wawili msichana na mvulana, akajisogeza ili apate kujua kama kuna lolote wanalolijua kuhusu mpenzi wake.
            Mara tu baada ya kuchana na Aidan pale kituo cha polisi Sunday akaenda moja kwa moja mpaka kwa Joyce na kumuelezea kuwa mpenzi wake yupo mikononi mwa polisi..wakaondoka wote kwa pamoja na kuelekea nyumbani kwa Aidani kwa ajili ya kuchungua nguo za kubadilisha na kumuandalia angalau kifungua kinywa.
            Akiwa amechoka kusubiri pale nyumbani kwa mpenzi wake mara anaona gari inakuja na kusimama usawa wa mlango wa nyumba ya Aidani, mazungumzo kati ya Winnie na watu wale wawili hayakuwa marefu kwani wao hawakuta kumjua, samahani jamani mimi nina shida na Aidani na nimemsubiri hapa kwa muda kidogo lakini hajatokea na simu yake haipokelewi, sasa sijui kama mtakuwa mnaelewa lolote linaloendela?..ndiyo yupo kituo cha polisi na hapa tumekuja kumchukulia nguo za kubadilisha na chai angalau akafungue kinywa, kwa hiyo kama una shida ya kumuona tunaweza kuongozana kuelekea kituoni ili ukamuone. Baada ya kukusanya nguo na kuandaaa chai wote watatu bila kueleweshana vizuri wanahusianaje na Aidani wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza…njiani kila mtu alikuwa kimya akiwaza yake, kutathmini na kung’amua mawazo ya mwanadamu mwenzako ni mtihani ambao hakuna mwanadamu ambaye amekwishafaulu mpaka sasa..walipofika kituoni wakapewa ruhusa ya kumuona na ndipo patashika ilipoanza. Winnie, akaanza kwa kuomba msamaha kwa mpenzi wake kwa yaliyotokea jana mpaka wakashindwa kuonana, ni kwamba alionana na dada yake na hivyo ikambidi aelekee nyumbi kwao.
            Joyce kusikia vile akaja juu bila kujua ni wapi alipo, varangati likaibuka..Joyce akitaka maelezo kutoka kwa Aidani juu ya uhusiano wake na Winnie, huku Winnie naye akimganda Aidani kutaka kujua ni nini kilichopo kati yake na Joyce…waswahili nyani haoni kundule, Winnie akasahau kabisa kuwa usiku wa kuamkia siku hiyo alikuwa katika himaya ya mkuu wake wa shule akimpa huduma ya mapenzi na sasa kinamuuma kujua kuwa mpenzi wake ana mpenzi mwingine. Joyce akamvagaa Winnie wakakamatana na ugomvi ukawa mkubwa..askari polisi wakawahi kuwatenganisha na bila kuulizwa kitu chochote wakawekwa rumande kwanza ili akili ziwatulie na wajue kuwa mahali walipo siyo pa mchezo na wala siyo disko kama ambavyo walidhani. Baada ya muda kupita wakatolewa na kila mmoja kuhojiwa ni kwanini wameamua kupigana kituoni?..maelezo yao yakawa kichekesho masikioni mwa askari polisi..ghafla mkuu wa kituo akaingia na kukuta mahojiano kati ya joyce na askari yakiendelea. Huku akionekana ni mwenye haraka akauliza
“..nini kinaendelea hapa”?.
“.ni hawa mabinti wameamua kuja kugombea bwana hapa kituoni kama vile wapo disko..”akajibiwa.
            Baada ya kuhutubia katika sikukuu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo ilikuwa ikifanyika mkoani hapo kitaifa, mheshimiwa waziri wa mambo yote akaendeshwa mpaka katika hoteli aliyofikia, na kutokana na tabia aliyojijengea ya kutolala peke yake alibiid aongee na dereva wake kuwa asikae mbali muda wowote atatkiwa kumpeleka sehemu akaonane na mtu muhimu. Baada ya kutafakari kwa makini ndipo alipoamua kumtafuta binti ambaye kwa mara nyingi amekuwa akilala naye mpaka asubuhi mara kwa mara alipofika mkoani kwa ajili ya shughuli binafsi au za kitaifa. Baada ya simu kuita zaidi ya mara tatu bila kupokelewa..akaamua kuwa sasa anapiga kwa mara ya mwisho na ispopokelewa ataangalia utaratibu mwingine.
“.halooo!!!!”
 upande wa pili sauti ikasikika
“…nahitaji kuongea na mwenye hiyo simu….” akaamrisha..hapa ni kituo cha polisi na mwenye hii simu anashikiliwa na polisi kwa utovu wa nidhamu hapa kituoni…ameleta fujo hapa
“…nahitaji kuzungumza na mwenye hiyo simu akasisitiza..fanya haraka kama unahitaji kuendelea kuwepo hapo kazini”……………ITAENDELEA
                                                                      

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...