Na Fredy Julius |
UTANGULIZI
Naomba
nianze kwa kusema kuwa, binadamu hawezi kuwepo bila ya mazingira kwa sababu
binadamu anategemea mazingira, mazingira yanaweza kuendelea kuwepo na kustawi
kwa miaka mingi ijayo kwa sababu mazingira hayamtegemei binadamu. Binadamu
anapoharibu mazingira anajiharibia nafasi ya kuendelea kuwepo katika mazingira
husika. Sasa basi kama sisi binadamu tunatamani na tunataka kuendelea kuonekana
katika uso wa hii dunia ni lazima na hatuna budi kuhakikisha kuwa tunatumia
nguvu zetu nyingi katika kutunza, kuhifadhi na kuendeleza ubora wa mazingira
haya kwa sababu bila ya kufanya hivyo maana yake ni kwamba tunatengeza
mazingira ya mahangaiko yetu wenyewe na hatimaye kufutika kabisa katika uso wa
hii dunia. Moja ya mambo ambayo yanaathiri maish ya binadamu kwa kiwangi
kikubwa ni uharibifu wa mazingira n akwa sababu asilimia kubwa ya wananchi
hawajui umhimu na uhusiano iliopo kati ya binadamu na mazingira hawaioni hatari
ambayo ipo karibu yetu kutokana na kuharibu mazingira yanayotuzunguka. Kitu
amabcho ni hatari kwa maisha yetu na ya vizazi vyetu vijavyo…………..SASA ENDELEA.
Hivi Chriss ni kwanini hawa ndugu zako wapo
hivi, mbona mambo wanayoyafanya ni tofauti kabisa na jinsi ambavyo wewe umekuwa
ukiwafanyia?. Hivi huyu si yule shangazi yako ambaye mwanae ulimsaidia
kumfundisha mpaka akafaulu vizuri kidato cha sita lakini yeye anakudharau kama vile huna mchango wowote katika maisha yake halafu
na wewe unaona ni sawa tu? Wala hupotezi muda wako kujiuliza ni kwanini na
ikibidi uwe unawaambia ukweli, mimi naona wanavyokutendea sio sawa kabisa
inabidi angalau wakuheshimu na kujali na kuthamini mchango ambao tayari
umeshatoa katika maisha yao.
Kwa sababu hata yule baba yako mdogo naye tabia zake sio nzuri. Ameamua
kukudhulumu kiasi kikubwa kabisa cha pesa lakini wewe hata hujali, hivi ni
kwanini uko hivyo wewe?
Hivi unanisikiliza ninyoyaongea au uko
mbali na hapa tulipo, maana naona hujibu kitu, akaamua kuuliza Ephraim baada ya
kuona rafiki yake yuko mbali kimawazo na ni kama
hamsikilizai maneneo anayoyaongea. “ nakusikiliza sana na nakuelewa
unayoyaongea, sema mawazo yangu yametekwa na kipindi kijacho cha bunge naona
kama tutachelewa kutazama nataka nijue ni mswaada gain utaletwa leo na nini
kauli za mheshimiwa wetu waziri wa mambo yote, ujue huwa simuelewi kabisa kiasi
nashindwa nimuweke upande gain, ni mzalendo kwelei au ni mnafiki tu nay eye ni
mmoja ya watu wanotafuna rasilimali za nchi hii bila kutazama jinsi wazee wetu
wanavyopata taabu huko vijijin”?. Sikiliza nikwambie rafiki yangu, hawa ndugu
zangu mimi nimeshawazoea sana na wala hwanipi tabu na nimeshamua na kukubali
kuwa wao ni wao na mimi ni mimi na kwa kawaida sipendi kujiuliza kwanini
sijalipwa fadhila za mema yangu ambayo nimeyatenda kwa mtu yeyote kwa sababu
naamini wao sio mimi kiasi watambue malipo ya wema.
Sasa nisikilize, wakati tunaendelea
kuzungumza naona ni vizuri tukaongeza mwendo ili tusichelewe kipindi cha bunge
cha jioni maana ni hamu sana na maneno ya wabunge juu ya huu muswaada uliowasilishwa,
yaani kuna wengine wanautetea kana kwamba hawaoni kuwa wanafuta maandishi ya
wino wanaadnika kwa kalamu ya risasi, halafu labda leo na mbunge anayewakilisha
jimbo letu naye anaweza kuongea watu tukamsikia maana tangu aende huko bungeni
hajawahi kuongea chochote na kama amewahi kuongea basi ni siku ambayo mimi
sikutazama televisheni au unasemaje? Kweli, rafiki yangu lakini mbona unamuita
mbunge anayewakilisha jimbo letu kwani wewe siyo mbunge wako? Kwanini usiseme
mbunge wetu? Waapi siwezi kusema mbunge wangu akati sikumpigia kura na wala
hakuna mwananchi ktoka katika jimbo letu ambaye alipiga kura ya kumchagua
mbunge, alipigiwa kura na watu wa chama chake akapitishwa sasa we unadhani
anamuwakilishaje mwamanchi ambaye hakumchagua? Yule yupo kule kuwakilisha jimbo
letu wala sio kuwakilisha wananchi maana hata mara moja sijawahi kusikia kuwa
amekuja kufanya mkutano na wananchi.
Haya
kaka, tuyaache hayo, rakini hata mimi nawasikia wananchi weengi tiu
wanalalamika juu ya huyu mbunge wa jimbo letu kuwa wamemchoka hata miaka mitatu
haijaisha, hivi kwanini tusifanye utaratibu wa wananchi kumbadilisha mbunge na
wamchague mwingine ambae wao wanahisi atawafaa? Hilo
ni sawa ila labda katika katiba hiyo mpya inayokuja maana hata kwa uelewa wangu
mdogo kuhusu sheria mbunge hawezi kubadilishwa na wananchi hata kama wananchi wao ndo wamempigia kura labda mpka mwenyeew
aamue kujiuzulu au chama chake kimfute uanachama maana katika katiba ya sasa
hakuna kipengele kianchoelezea kuwa wananchi wananweza kumuondoa mbunge katika
nafasi yake. Haya ya kuhusu ukomo wa mbunge kushika nafasi yake katika katiba
ya sasa yameelezwa katika ibara 71 kifungu cha kwanza kama ifuatavyo; 71 (1)
mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika bunge litokeapo lolote
kati ya mambo yafuatayo; (a) ikiwa litatokea jambo lolote amabalo, kama
asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteza sifa za
uchaguzi au asiweze kuchaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba
hii. (b)Ikiwa mbunge huyo atachaguliwa kuwa raisi (c) Ikiwa mbunge atakosa
kuhudhuria vikao vya mikuatano ya bunge mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya
spika. (d) Ikiwa itathibitishwa kuwa amevunja masharti ya sheria ya viongozi wa
umma. (e) Iwapo mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa makam wa raisi (f)Iwapo
mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au
alipoteuliwa kuwa mbunge (g) Kwa mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya
mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko
rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi
kwa ajili hiyo kwa mijibu wa sheria iliyotungwa na bunge,
lakini iwapo mbunge hatakoma kuwa mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati
ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi basi
mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama mbunge mpaka wakati bunge
litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila kuathiri haki na stahili
zizotoka na ubunge wake.
Sasa Ephraim hembu niambie, kwa mujibu wa
katiba jinsi ilivyo, we unadahini mbunge anawajibika kwa wanacnhi kweli au
anawajibika kwa chama chake ambacho ndio kimempa nafasi ya kugombea na kuwa
mbunge? Haya achana na hao wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi angalau
kidogo wanaona haya hata kwa maneno na lawama za wananchi kila kukicha juu ya
ugumu wa maisha. Hivi kwa mbuge anayewakilisha jimbo letu, kweli kabisa
atawajibika kwa wananchi ambao hata kumachagua hawakumchagu na hawana mamlka
kwa mujibu wa katika ya kumuwajibisha, au atawajibika kwa chama chake hiki cha
mageuzi amabcho ndio kilichomteua na kupelekea yeye kuwa madarakani kwa kupita
bila ya kupingwa, yaani hata kumpigia kura ya kuwa au ktukuwa na imani naye ili
kumthibitisha kuwa ndio mbunge wa wanachi wa jimbo hili hamna halafu tunataka
awajibike kwa wananchi, kweli inawezekana?.hapana.
Chriss hapo hata mimi naona kama mbunge sio
wetu bali ni wa chama ambacho ndio kimempa madaraka na kina uwezo wa
kumnyang’anya madaraka hayo, hapo kwa vyovyote ni lazima mbunge awajibike kwa
chama chake, hiyo iko wazi. Sasa umeona? Achana na huyu wa jimbo letu, je hawa
wa kuteuliwa watawajibika kwa nani ikiwa hawachaguliwi na wananchi? Kwa
vyovyote vile ni lazima watawajibika kwa chama chao na ndiuo maana utawaona
wabunge wa kuteuliwa wa chama tawala wanashabikia sera na mipango amabayo haina
mantiki wa tija kwa maendeleo ya taifa hili hata kidogo, maswali ya msingi nay
a nyongeza wanayoyauliza hayaeleweki na wanaongoza kwa kuwasifia mawaziri,
utasikia “ namshukuru sana muheshimiwa waziri kwa majibu mazuri na yenye kuleta
tija, na kwa kuwa naamini serikali ya chama changu ni sikivu basi naamini haya
yatatendewa kazi, lakini hata hivy muheshimiwa spika nina swali dogo moja la
nyongeza, kwa kuwa ni tangu mwaka juzi serikali imewaahidi wanachi wa mkoa
wangu kuwa misaada na mikopo kwa akina mama na wajasiliamali wadogowadogo
itafikishwa moja kwa moja kwa wahusika, na kwa kuwa wahusika wanalalamika kila
siku kuwa mpaka leo hawajapata hayo mabilioni tangu yalipotolewa, sasa je, ni
lini mheshimiwa wazri atawawajibisha watendaji wake na kuwaagiza kuwa wahakikishe
wanapeleka pesa hizo moja kwa moja kwa wananchi badala ya kupitishia katika
mtirirIko huo ambao unasababisha ubabaishaji mwingi na hatimaye wanachi wengi
wa hali ya chini kuzikosa pesa hizo”?. Sasa hapa utajiuliza uhalali wa kusifia
majibu yaliyotolewa na waziri pamoja na kuuliza swali la nyongeza kama hilo……………….ITAENDLEA WIKI
IJAYO
MAONI, 0766948187
No comments:
Post a Comment