Kwa ufahamu wangu finyu ukiniuliza kwa nini TANESCO wailipe DOWANS Tanzania Limited bilioni zetu 94 ntakupa majibu haya
1..sheria zetu butu juu ya makampuni ya wageni na wawekezaji
2..Tanesco walikubali kusaini mkataba wenye kifungu kinachowafunga kuwa maamuzi ya ICC ndo ya mwisho na hayatakuwa na rufaa na bila kufikiria maamuzi gani yatafanywa na ICC iihali wanajua kuwa DOWANS ni kampuni tata.
Tanesco ambao waliingia mkataba na Dowans Tz limited ambayo ilirithi mkataba toka kwa Dowans Holdings SA ya Costa Rica ambayo ilirithi mkataba huo toka kwa Richmond Development, walikuwa wanajua kabisa kuwa wanaingia mkataba na kampuni ambayo tayari ina utata na imeshaisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi
Chadema wameamua kuipa serikali siku 30 tangu octoba 8 kusitisha malipo hayo kwa Dowans vinginevyo watalipeleka suala hilo kwa wananchi walifanyie maamuzi, hili linakuja baada ya mahakama kuu ya Tanzania kuiamuru Tanesco iilipe Dowans kufuatia kuwepo kwa kufungu ambacho kilikataza chombo chochote cha sheria kuingilia au kutoa maamuzi juu ya mkataba huo, kwamba maamuzi ya ICC ( mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ) kuwa ndio yatakuwa ya mwisho na hakutakuwa na kukata rufaa…kusainiwa kwa mkataba huo inamaanisha kuwa Tanesco walikuwa na imani kuuubwa na ICC kiasi cha kuamini kuwa maamuzi yake yatakuwa ya haki lakini leo maamuzi hayo yanatupa kizungumkuti watanzania…
Maswali ya kujiuliza ni haya
1. Tanesco walifanya maamuzi ya kizalendo?
2. Sheria zetu zina utetezi gani juu ya maamuzi yaliyofikiwa?
3. Nini kauli na msimamo wa serikali juuu ya malipo hayo, ikiwa baadhi ya watendaji wa serikali wanakili kuwa dowans ni wahuni?
4. .Nini wamefanywa mpaka sasa watendaji wa taneco waliopelekea kizungumkuti hiki?
Binafsi sitamani hata kidogo kushuhudia Dowans wakilipwa mabilioni haya ya wavuja jasho..msimamo wa Samwel Sitta akiwa ni mtendaji wa serikali kwanini usiwe msimamo wa wenzie waliomo katika serikali hiyo hiyo na hatimaye kuwa msimamo rasmi wa serikali?
2 comments:
me bado ubongo wangu umeganda juu ya haka kamchezoo
kama vipi itabidi tanesco tuiuze kwa dowans
Post a Comment