FOLLOWERS

Monday, July 16, 2012

HADITHI : NDOTO YA PENZI SEHEMU YA 01

Na Fredy Julius


NDOTO YA PENZI SEHEMU YA 01 na Fredy Julius
UTANGULIZI
Hakuamini macho yake wala masikio yake kuwa kama ni kweli yote aliyoyaona yalikuwa katika ndoto. Benny akamuuliza tena Caroline..”ni kweli nilikuwa naota..? siamini mpenzi wake..yaani sitaki kuamini hata kidogo!! Yaani siamini mpenzi kama kweli hii ni ndoto tu. Benny akamkumbatia Caroline kwa nguvu zake zoote kama vile alihisi kuwa atamponyoka, huku machozi yakimtoka akamwambia Caroline nakupenda!..Nakupenda ten asana kuliko vile unavyofikiria na nitakupenda daima, sidhani kama atakuja tokea mwingine kama wewe. Hii ndoto ya penzi langu kwako nahisi ipo siku itakamilika,nitakuja kufa kwa ajili yako caroline……….Sasa endelea

            Ni baada ya makubaliano kati yao wawili yaani Benny pamoja na Caroline kwamba wakati muafaka wa wao kufunga pingu za maisha ulikuwa umewadia, ndipo Benny alipofuata taratibu zote na mila na desturi za mtanzania ili aweze kuweka jiko ndani. Ilikuwa ni siku tatu tu kabla ya ndoa yao pale Benny alipokwenda kijijini kwao kuwataarifu baba na mama yake kuhusu shughuli hiyo ya ndoa ambayo walitarajia kuifanyia mjini, siku hiyo ya ndoa ambayo alikuwa ameipangilia vibaya mno.
            Baada ya masuala yote kuisha kijijini kwao na kukubaliana na wazazi wake kuwa kesho yake wangekuwa safarini kuelekea mjini kwa ajili ya maadalizi ya shughuli ya mwanao mpendwa ndipo alipofunga safari kurejea mjini kuendela na shamra shamra nyingine za maandalizi ya harusi hiyo. Wakiwa wamezoeana na wanapendana sana Benny na Caro ilikuwa inakuwa vigumu mno kwa mmoja kupitisha siku kadhaa bila kumuona mweziye, akarejea nyumbani na kumkuta kipenzi chake Caro akimngoja kwa hamu, hadithi za kuhusu shamba zilikuwa chache kutokana na uchache wa siku ambazo alikaa kijijini. Baada ya mazungumzo caro aliandaa chakula na kuamua kuwa wale pamoja mchan huo na baada ya hapo atakapoondoka kurejea nyumbani kwao kuja kupika tena katika jikola Benny ni mpaka atakapokuwa mke halali, si kupika tu bali ilikuwa akiondoka hapo kuonana tena ni mpaka kanisani siku ya kufunga ndoa.
            Meza ikaandikwa na wapendanao maharusi watarajiwa wakajongea mezani kwa ajili ya chakula cha mchana..vipi chakula mpenzi wangu?..unakionaje, Caro akamuuliza Benny..mmhhh!!! kitamu sanaa Caro wangu, alimjibu huku akibugia mnofu wa nyama mdomoni.mazungumzo ya hapa na pale kati ya wawili hawa yakaendela huku wakila chakula chao kwa furaha na upendo. Baada ya kumaliza kula Benny akatoa vyombo mezani na kwenda kuviosha…na nataka hata ukishanio uwe na moyo huu wa kutoa vyombo na kuviosha, siyo unajifanya leo una mzuka halafu nikija huku ndani iwe ndo kijakazi wakooo..akamtania Caro..wala hata usijali bosi wangu, mimi kwao tena?,,si unajua mimi ni mtumishi wako..sema lolote bosi nami mtumishi wako nitatekeleza, leo, kesho na hata milele.
            Wakiwa juu ya sofa pale sebuleni, Caro alikuwa akimuaga Benny..Benny nae akimg’ang’ani Caro aendelee kubaki japo kwa muda kidogo hamu yake kidogo ipungue..khaaa bosiii ujue ukiondoka hapa ndiyo sikuoni tena mpaka wakati wa harusi?..ndiyo hivyo asa we unataka nikae hapa mpka saa ngapi mpezi wanguu, giza limeshaanza kuingia acha tu niende bwana..hata mimi nitakumiss sana Benny wangu..Bosii kaa basi kidogo hata dakika ishirini hivi halafu ndiyo uondoke au vipi?..acha mimi niende mpenzi wangu..kuja kidogo tu imekua taabu, si unajua kuwa nimetoroka tu home?..sasa wataanza kusema vibaya bwanaaa!!...Wakiwa bado pale juu ya sofa wakibadilishana mawazo na kuendeleza mabishano yao kimahaba mahaba ..Mara ghafla mlango ukafunguliwa na watu wanne wakaingia ndani..wakabaki wameduwaa juu ya sofa wakiwatazama kwa hamaki wasijue nini cha kufanya……… itaendela wiki ijayo

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...