FOLLOWERS

Friday, October 28, 2011

KENYA NA OPARESHENI YA KUWATOKOMEZA AL-SHABAB

 Baadhi ya wanamgambo wa Al-Shabab wakiwa na siraha mikononi tayari kwa ajili ya mapambano


 Wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabab wakiwa katika moja ya misafara yao ya kila siku


 Wanamgambo wa kukundi cha Al-Shabab wakiwa wamepumzika, kenya wanahaha usiku na mchana kuwatokomeza wanamgambo hawa


Wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabab wakiwa katika mafunzo ya jinsi ya kutumia na kulipua makombora kama wanavyoonekana katika picha. Kenya wanahaha usiku na mchana kuwatokomeza wanamgambo hao kufuatia muendelezo wa mashabulio ya mabomu katika jiji la nairobi ambayo yanaripotiwa  kufanywa na wanamgambo hao.


Majeshi ya Kenya yameendelea na msako wa kuwasaka wanamgambo wa kikundi cha Al-shabab ambacho kinasadikika kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kufuatia kutekwa nyara kwa raia wa kifaransa aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la misaada la umoja wa mataifa. Oparesheni hiyo ambayo inaendeshwa na Kenya katika nchi ya Somalia imefuatiwa na utata baada ya raisi wa Somalia kudai kuwa hawakutoa ruhusa kwa Kenya kuendesha oparesheni ya kijeshi katika nchi hiyo na papo hapo ikafuatiwa na mashambulio matatu katika jiji la Nairobi ambapo katika shambulio la jana basi lililokuwa na maafisa wa elimu wa Kenya waliokuwa katika harakati za kusimamia mitihani ya nchi hiyo lilishambuliwa mpakani mwa Kenya na Somalia na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine kujeruhiwa vibaya…swali ambalo watu wengi bado wanajiuliza ni je Kenya watawaweza Al-shabab au wamewasha moto ambao utawashinda kuuzima?..pamoja na hayo ufaransa imeahidi kuisaidia Kenya katika oparesheni hiyo ya kutokomeza kikundi hicho cha wanamgambo wa Al-shabab

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...