FOLLOWERS

Thursday, August 9, 2012

HADITHI : NDOTO YA PENZI SEHEMU YA 03

na fredy julius
ILIPOISHIA
 
Risasi tatu zilimpata sawia Benny, moja bega la kushoto, moja mbavu za kulia na nyingine tumboni akagaa gaa chini kwa maumivu makali akapoteza fahamu, giza tupu mbele ya macho yake. Muungurumo mkubwa wa gari na kasi ya kuondokea ndiyo vitu vilivyomshtua mpangaji mwenzake mwanadada Mercy na kutaka kujua kulikoni, akatoka mbiyo kuelekea chumbani kwa benny ili akajue kulikoni. Mbio mbio hadi chumbani kwa Benny, alimanusura azimie kwa hamaki.!!!baada ya kuushuhudia mwili wa Benny ukiwa unaogelea kwenye kajidimbwi kadogo ka damu pale sebuleni…akiwa ametaharuki akapiga hatua mbili tatu akainama kifuani pa Benny ili asikilize mapigo yake ya moyo kama bado yanaendela, ile kuugusa mwili na kugundua kuwa moyo wa Benny bado ungali unafanya kazi yake ijapokuwa ni kwa umbaali sanaa, akapigwa na butwaa tena kusikia hodi inapigwa mlangoni….akachanganyikiwa asijue nini la kufanya…akaamini kabisa ni polisi na sasa ni lazima atawajibika kwa sababu ya kifo cha Benny..akahamaki!!!...SASA ENDELEA

Kuhusishwa na kifo cha Benny mtu ambaye hakuwahi kudhani kuwa anaweza kuwa na maadui kiasi wafikie maamuzi ya kumuua…bila yeye kuwa amehusika wala kuona wala angalau kuelewa kitu chochote juu ya tukio hilo..Mercy akazidi kuchanganyikiwa..akabaki ameduwaa akijiuliza nini cha kufanya……
Akiwa bado kapiga magoti pale chini, kamkamata Benny…La hashaa!! Kumbe walikuwa ni baba na mama yake Benny tayari walikuwa ndani ya sebule baada ya kungoja kufunguliwa kwa muda wakaamua kuusukuma mlango na kuingia ndani ya nyumba. Tayari walikuwa ndani ya sebule huku wakiwa hawaamini kile walihokuwa wakikishuhudia kwa macho yao, mbele yao…mama mtu akadondoka chini na kupoteza fahamu wakati baba yake Benny bado haamini macho yake kile alichokuwa akishuhudia mbele yake.
Akiwa bado haamini maco yake, ndipo mercy alipozinduka kutoka katika lindi lile la mawazo na haraka haraka akachukua simu yake ya kiganjani na kubonyeza namba kazaa kasha akaonekana kungoja…..simu iliita kwa muda bila majibu yeyote toka upande wa pili..akarudia tena…ikaiita bila kupokelewa..akarudia tena…ikaita kwa muda kasha ikapokelewa..haloo!!..halooo!!! ni kituo cha polisi hapo?..ndiyo, tukusaidie nini binti?..kuna uvamivizi umetokea huku mitaa ya kaloleni karibu na kanisa la RAGTna kuna mtu amejeruhiwa vibaya sana tunahitaji msaada wa polisi…Ok sawa askari wetu watafika hapo muda siyo mrefu baada ya kurudi kutoka katika tukio lingine walilokwenda kushughulikia…baada ya polisi Mercy akapiga simu hospitali na kuomba msaada wa gari la wagonjwa.
Muda si mrefu ambulance na gari la polisi zilfika kwa pamoja kana kwamba zilitoka sehemu moja,         miili ya Benny na mama yake ilipakiwa ndani ya gari lile la wagonjwa tayari kwa kuelekea hospitali kupata huduma za kitabibu. Mercy akachukuliwa ndani ya gari lapolisi tayari kwa kuelekea kituoni kutoa maelezo kuhusu tukio lote jinsi lilivyotokea na mzee Mwita yaani baba yake Benny akaongozana na gari la wagonjwa kwa ajili ya kuwa karibu na wagonjwa kule hospitali.
Musa anafika kwa Mercy na kukuta gari la polisi ndiyo linaondoka naye..kumtazama mpenzi wake akaona analia…naye machozi yakaanza kumlenga lenga pasipo hata kujua ni nini hasa kinamliza mpenzi wake…ikabidi papo hapo naye ageuze kuanza kulifuata gari la polisi kuelekea kituoni ili akajue kulikoni mpenzi wake kakamatwa?
 Range rover lile jeusi liliendeshwa kwa mwendo ule ule wa kasi moja kwa moja mpaka mbele ya geti moja kubwa sana jeusi…lile geti kufunguliwa tu Caro alishuhudia vijana wengine wanne wenye afya zao za maana kama wale aliokuwa nao ndani ya gari na mbele yale kulikuwa na jumba kubwa la kifahari la kuishi lenye ghorofa moja na ilionekana dhahiri kuwa wanaoishi ndani ya jumba lile ni watu na pesa zao na pia wameshikilia baadhi ya sekta za serikali. Hii ni kutokana na kumshuhuda kwa macho yake Inspecta Jenerali wa polisi akitoka ndani ya jumba lile na kupishana nao kasha akaingia ndani ya gari lake alilopewa kwa dhamana ya kodi za wananchi na kuondoka zake.
Baada ya kufikishwa pale kituo cha polisi, Mercy anajikuta katika wakati mgumu mikononi mwa polisi baada ya kutoa maelezo yake pale polisi ndani ya chumba kilichokuwa na kibao kilichoandikwa Criminal Investigation Departiment (CID). Inspekta wa kituo kile cha polisi akaamuru awekwe rokapu kwa ajili ya kuisaidia polisi katika upelelezi wa kesi hiyo.
Muda si mrefu Musa naye akawasili ktuo cha polisi akiwa na kihoro cha kutakakujua kulikoni mpenzi wake akakamatwa….enheee!! wewe vipimbona unahema bila sababu sema tukusaidie nini?...afande mimi naitwa Musa..nimekuja kumuangalia mpenzi wangu amekamatwa na polisi muda siyo mrefu mitaa ya kanisa la RAGT….enhee kwa hiyo?..ndiyo hivyo afande nataka kumuangalia…sijui ni kwanini amekamatwa..utajua kwani wewe ni yeye?..yeye anajua ni kwa nini amekamatwa bwana mdogo embu ngoja hapo katika benchi.
Wakati hayo yanaendelea kule hispitali baba yake Benny akiwa amechanganyikiwaasijue nini cha kufanya mkewe anapata fahamu na baada ya kutulia kwa muda mfupi akaanza kusisitiza kuwa anataka kumuona mwanaye hata kama amefariki wamuonyeshe maiti yake ndipo akili yake itatulia..akachukuliwa moja kwa moja hadi katika chumba cha wagonjwa mahututi Intensive Care Unit (ICU) na kumkuta Benny akiwa katika mashine maalum ya Oksijeni ili kumsaidia kupumua mama kuona vile akaishiwa nguvu akaanguka tena.
Akiwa ametulia katika benchi lile huku lindi la mawazo likiwa limemchukua mara akasikia sauti za kwikwi za kilio, kuinua macho akamshuhudia Mercy akiwa ameongozana na askari wengine watatu mikononi amafungwa pingu….khaaah!! afande mtu ninyetaka kumuona ndiye huyu hapaa..sasa wanampeleka wapii tenaa jamanii?/..mbona sielewi elewi kinachoendelea hapa??....eti Mercy mama kuna nini?..umefanya kosa gain mbona mimi sielewi?..jamani afande kuweni na huruma basi…Musa maneno yalimtoka pasipo yeye mwenyewe kujijua…askari wakasimama wakiwa wametahayari na wao..kwani kuna nini hapa afande John?..ni huyo dada..huyo hapo ni mpenzi wake kaja kumuona sasa tulikuwa tumemwambia angoje hapo katika benchi mkimaliza kuhojiana naye tupate kumruhusu amuone..kwani mnampeleka wapi?..huyu anaenda jela..haruhusiwi kupewa dhamana mpaka upelelezi wa hii kesi ukamilike ndivyo mkuu alivyotuagiza.
Kwa hiyo ndiyo manmpeleka?..ndiyo?..basi kama ndiyo hivyo wapeni nafasi  hata ya dakika kumi tu waambiane ni nini kimetokea maana bwana mdogo hapa anaonekana hajui mpenzi wake amefanya nini mpaka akafikishwa hapa..hayaa tunawapa dakika kumi tu hatuna muda wa kupoteza isitoshe tukikutwa hapa mnaongea itakuwa balaa…wakasogea pembeni..mama vipimbona naona mauza uza tuu?..kun nini kimetokea nambie..sikia mpenzi wangu Musa nikwambie..Benny yule kaka anayekaa mlango unaofuta baada ya wangu kavamiwa mchana huu kapigwa risasi na sidhani kama atapona. Khaaa!! Kweli?..ndiyo hivyo…acha utani mercy sasa wewe unahusikaje hapo?na mbona muda siyo mrefu tulipokuwa tunaongea ulionekan uko kawaida na hakuna lolote baya..yaani muda mchache wa mimi kutoka nyumbani kuja kwako ndiyo yametokea yote hayo?
Musa.wewe si unamjua caro mpenzi wake Benny?..ndiyo..sasa ilikuwa hivi..mimi ninapotoka sokoni kununua mboga na vitu vingine nilikuta gari aina ya vogue jeusi limepaki mlangoni kwa Benny, kwa sababu najua kuwa Caro kwao wana uwezo nikajua atakuwa ni yeye kaja nalo ukizingatia ni siku chache sana kama tatu hivi zimebaki kabla ya ndoa yao..ndiyoo!!..enhee nilipoingia ndani nikaanza kuandaa mboga ndiyo wewe ukanipigia simu..akaendelea kumsimulia mpenzi wake huku machozi yakimtoka na kwikwi zikiendelea..nilipomaliza kuongea na wewe nikasikia ile gari inaondoka kwa kasi ajabu..nikashtuka nikatoka..kutoka nikakuta ndiyo inapotelea kwenye ile kona pale nyumbani.
Caro akajua kuwa mpaka hapo alipofikishwa ni ndoto kubwa sana kwake kutoka na hatimaye kuja kutimiza ndoto yake ya kufunga pingu za maisha na Benny..akaanza kulia….machozi yakamtiririka…lakini hakukuwa hata na mtu mmoja aliyejali chozi lake..chozi lamnyonge hulipwa na mungu. Upande wake wa kulia alishuhudia gari kama nane hivi za kifahari na alipogeuka kushoto alikutana uso kwa uso na uso wa kijana mtanashati uliokuwa umejaa tabasamu tele kana kwamba walikuwa pale kwa ajili ya kufanya pati ya hapy birthday…huyu si mwingine bali Innocent aliyewhi kumtongoza caro mara kwa mara lakini yeye akamkataa kata kata..alikuwa amezungukwa na vijana wengine kama wanne hivi waliokuwa na vyombo vya moto mikononi mwao..akataharuki!!!....itaendelea

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...