FOLLOWERS

Sunday, November 3, 2013

MIKASA YA MAPENZI : MPE USHAURI HUYU KAMFUMANIA MPENZIWE

Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mchumba tuliyedumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.

Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014 na utambulisho tayari umefanyika.


Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenzi wake wa zamani ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.


Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.


Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenzi wake wa zamani analala kwake siku ambayo mimi sijaenda. Juzi nikapigiwa simu na majirani zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia simu kuwa 'nataman kuwa nawe leo' akaniambia nimechoka kweli naona tuonane kesho. Mimi nikaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic.


Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki:

1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikana kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.

Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini

1 comment:

Unknown said...

Njoo kwangu cjaoa

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...