FOLLOWERS

Tuesday, July 17, 2012

HADITHI : NDOTO YA PENZI SEHEMU YA 02

Na Fredy Julius

NDOTO YA PENZI SEHEMU YA 02 na Fredy Julius
ILIPOISHIA
`Wakiwa juu ya sofa pale sebuleni, Caro alikuwa akimuaga Benny..Benny nae akimg’ang’ani Caro aendelee kubaki japo kwa muda kidogo hamu yake kidogo ipungue..khaaa bosiii ujue ukiondoka hapa ndiyo sikuoni tena mpaka wakati wa harusi?..ndiyo hivyo asa we unataka nikae hapa mpka saa ngapi mpezi wanguu, giza limeshaanza kuingia acha tu niende bwana..hata mimi nitakumiss sana Benny wangu..Bosii kaa basi kidogo hata dakika ishirini hivi halafu ndiyo uondoke au vipi?..acha mimi niende mpenzi wangu..kuja kidogo tu imekua taabu, si unajua kuwa nimetoroka tu home?..sasa wataanza kusema vibaya bwanaaa!!...Wakiwa bado pale juu ya sofa wakibadilishana mawazo na kuendeleza mabishano yao kimahaba mahaba ..Mara ghafla mlango ukafunguliwa na watu wanne wakaingia ndani..wakabaki wameduwaa juu ya sofa wakiwatazama kwa hamaki wasijue nini cha kufanya……… SASA ENDELEA
                        Kufumba na kufumbua, watu wanne wenye afya haswaa ndani ya suti za thamani nyeusi, miwani mieusi machoni na kofia nyeusi aina ya pama walikuwa wamesimama ndani ya sebule mbele yao wakiwatazama kana kwamba walikuwa wanauliza swali..mbona mnatushangaa?. Wakatoa bastola zenye viwambo maalum vya kuzuia sauti na kuwaamuru kutulia kimyaa kama wanakondoo..Kiongozi wa msafara ule wa mijitu ile minne “Lenny” akamsogelea kwa dharau Benny ambaye muda huo alikuwa amesimaa tayari kwa lolote na kumkata kofi ziti la katikati ya paji lake la uso..akagugumia kwa maumivu makali..akiwa haoni mbele na anayumba yumba mithili ya mlevi aliyelewa kimpumu akajikuta anabwagwa chini kama gunia baada ya kukatwa bonge la mtama na kudhibitiwa vilivyo chini ya uangalizi mkali wa vijana HB na Snizor. Maumivu juu ya maumivu..kwa mbali akawa anasikia sauti ya kipenzi chake caro ikilia kwa uchungu..kutaka kuinuka lilikuwa kosa kubwaa mnoo..akapigwa ngumi nzito ya chembe iliyompeleka mpaka chini, na kwa mara nyingine akagugumia kwa maumivu matamu.
            Wazazi wake wakiwa wenye furaha tele, baada ya maandalizi na kila kitu kukamilika kule kijijini wakashika njia kuelekea mjini tayari kwa kushuhudia ndoa ya mtoto wao wa pekee Benny, ambayo walitegemea ingefungwa baada ya siku tatu kutoka siku hiyo wakiwa wanasemezana kwa furaha na kutabiri ni jinsi gain watapendeza siku hiyo ya harusi ya kijana wao na jinsi watakavyorudi kufanya sherehe kuubwa ya kuimba na kucheza ngoma pale kijijini ili kuwafunga midomo wambea wote wa kijiji waliendelea na safari yao kuelekea mjini bila kujua kuwa wanakoelekeea kuna matatizo makubwa na wala sir aha kama mawazo yalivyo vichwani mwao.
            Lenny alimbeba Caro mzobe mzobe hadi nje kwenye gari range rover nyeusi, kioo tinted nyeusi akiwa amefungwa plasta mdomoni ili asipige kelele na kuwashtua majirani ambao hawahusiki na mchezo huo. Ndani ya  gari akapokelewa na kijana Tino na kuwekwa katika ulinzi mkali. Akarudi ndani..tumfanyeje huyu bwege?...akawauliza wenzake…kama vipi tummalize kupoteza ushahidi..akajibu Snizor…lenny akatoa bastola kiunoni mwake na kumtandika risasi tatu mfululizo kasha wakatoka na kuwasha gari na kutokomea kusikojulikana katika mwendo wa kasi.
            Mercy hakuwa na shaka hata kidogo baada ya kuliona gari aina ya range rover limepaki sawia na mlango wa Benny, kwani licha ya kuwa yeye binafsi alikuwa na kipato cha kawaida ambacho kamwe kisingeweza kumuwezesha kununu hata Vitz, Mercy aliyatambua fika mahusiano kati ya Benny na Caron a pia alielewa wazi kuwa familia ya akina Caro ni familia ambayo inajiweza kifedha na si mara moja amemshuhudia akija hapo kwa mpenzi wake kwa kutumia gari za gharama. Leo ni siku kadhaa kabla ya ndoa, hakutaka kujiuliza maswali mengi wala kuwaharibia starehe wanaharusi hao watarajiwa, akapitiliza zake chumabi kwake.
            Benny na Mercy ni wapangaji ambao wamezoena na wanataniana sana, wanasaidiana katika mambo mengi kwani licha ya ukweli kuwa wamepanga katika nyumba moja lakini wao pia ni watu ambao wamesoma katika shule moja ya sekondari kwa muda miaka mine katika shule ya sekondari mtakatifu neema. Wanaheshimiana kutokana na ukweli kuwa kila mmoja alimfahamu vizuri mwenzie ni mtu wa aina gain, hapendi nini katika wakati gain. Mercu akaingia ndani…nyanya, vitunguu,pilipili hoho, bamia akaviweka sawa ilia nayeye aanze mapishi..simu ikaita.
            Haloo!!..mambo vipi mpenzi wangu, alikuwa ni Musa mpenzi wake wa siku nyingi tangu akiwa shule ya sekondari ya mtakatifu neema, pouwaa..mpenzi wangu vipi mzima wewe lakini?..mimi mzima mama angu…vipi umeshapika?..mi ndiyo kwanza nataka nianze kuandaa mboga hapa… Ok poaaa!!! Sasa fanya hivi, achana na hizo shughulizako za kuandaa mboga mimi nakuja sasa hivi nikuchukue hapo tukape lunch wote kwa pamoja.then baada ya hapo nitakurudisha nikupikie hizo bamia zako halafu mi nitarudi kwangu au siyo mamaa!!..pouwaaa mpenzi basi acha nijiandae hapa..niupare mtoto wa kike ii ukija kwanza unikute tayari halafu ukiniona tu unitamani mwenyewe na roho yako…pouwaa baadae kidogo basi..ookk pouwaaa babaa nakungoja.
            Risasi tatu zilimpata sawia Benny, moja bega la kushoto, moja mbavu za kulia na nyingine tumboni akagaa gaa chini kwa maumivu makali akapoteza fahamu, giza tupu mbele ya macho yake. Muungurumo mkubwa wa gari na kasi ya kuondokea ndiyo vitu vilivyomshtua mpangaji mwenzake mwanadada Mercy na kutaka kujua kulikoni, akatoka mbiyo kuelekea chumbani kwa benny ili akajue kulikoni. Mbio mbio hadi chumbani kwa Benny, alimanusura azimie kwa hamaki.!!!baada ya kuushuhudia mwili wa Benny ukiwa unaogelea kwenye kajidimbwi kadogo ka damu pale sebuleni…akiwa ametaharuki akapiga hatua mbili tatu akainama kifuani pa Benny ili asikilize mapigo yake ya moyo kama bado yanaendela, ile kuugusa mwili na kugundua kuwa moyo wa Benny bado ungali unafanya kazi yake ijapokuwa ni kwa umbaali sanaa, akapigwa na butwaa tena kusikia hodi inapigwa mlangoni….akachanganyikiwa asijue nini la kufanya…akaamini kabisa ni polisi na sasa ni lazima atawajibika kwa sababu ya kifo cha Benny..akahamaki!!!...
Kuhusishwa na kifo cha Benny mtu ambaye hakuwahi kudhani kuwa anaweza kuwa na maadui kiasi wafikie maamuzi ya kumuua…bila yeye kuwa amehusika wala kuona wala angalau kuelewa kitu chochote juu ya tukio hilo..Mercy akazidi kuchanganyikiwa..akabaki ameduwaa akijiuliza nini cha kufanya……itaendeleea

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...