Aliongeza kuwa wananchi wa eneo la Kidugalo mwaka jana wamefyatua na kuchoma tofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwamba hivi sasa kinachosubiriwa ni nguvu toka serikalini kutoa vifaa vya kiwandani ili kuweza kufanikisha kupunguza kero hiyo ya muda mrefu.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini. ( CHANZO : JAMII FORUMS)