FOLLOWERS

Thursday, August 9, 2012

BENKI YA KIISLAMU YA WATU WA WANZIBAR (PBZ) WAFUTURU NA MAKAMU WA RAISI

 Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari  iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana  na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu  pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...