FOLLOWERS

Monday, July 16, 2012

AJALI STENDI YA MAKAMBAKO

Basi la Prince Muro likiwa nyuma ya basi la sai baba baada ya kulivamia kwa nyuma kutokana na kuhofia kuligonga roli..halipo pichani

abiria waliokuwa wakisafiri na mabasi hayo wakiwa wametoka nje wakiwasubiri askari wa usalama barabarani kwa ajili ya taratibu za kiuchunguzi

abiria na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo
Ajali ya mabasi imetokea nje kidogo ya stendi kuu ya mbasi ya Makambako yanayo kwenda Mbeya yakitokea Dar. Ajali hiyo imetokea mida saa 11 jion, wakati basi la Sai baba likiwa linataka kupita lori lililobeba mawe kwenye matuta yaliko karibu na hiyo stend. Basi la Sai baba lilifunga breki kwa ghafla kwa kuhofia kuligonga lori hilo huku nyuma yake kukiwa na basi la Prince Muro ambalol ilikuwa ngumu kwa dereva kufunga breki ya ghafra ili asiligonge basi la Sai baba na hivyo kulivaa kwa nyuma.
Aidha katika ajali hyo hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa  bali ni uhalibifu uliotokea katika gari la Sai baba kwa kuvunjika kioo cha nyuma na basi la Prince Muro kuvunjika side mirror.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...