Kama ingetokea taifa stars ikaifunga Moroco katika mechi yao ya mwisho ya kufuzu katika michuano ya mataifa huru ya afrika yatakayofanyika mwakani huko Guinea bila shaka Tanzania ingelipuka kwa shangwe na furaha zisizo na kifani, lakini hali ikawa tofauti na maombi na dua za wengi. Bado huwa nakumbuka bao lililofungwa na Erasto Nyoni na kuiondoa Burkinafaso katika michuano ya afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani
Burkinafaso walituzidi kwa kila kitu nabado huwa naamini ile ilikuwa ni ndondokela au tuseme bahati nasibu kama ambavyo ingeweza kutokea kwa Moroco lakini hali ikawa tofauti tukaambulia kipigo cha 3-1
Umefika wakati ambapo watanzania wote na TFF kujua kuwa kila kitu huanzia chini, huwezi kufika kumi bila kupita tisa, kama tupo namba moja tukubali kuwa tunasafari kuubwa ya kuzipita namba hizo tisa zilizopo hapo mapka kufikia kumi. Ni muhimu kwa TFF sasa kuanza kutengeneza timu za vijana ambazo zitakuwa na misingi thabiti kisoka na tuachane na hizi habari za kung’ang’ana na wachezaji ambao hawawezi kucheza kombe la dunia 2014 Brzili tutakapokuwa tumefuzu, tutengeneze timu ambayo itacheza 2014, 2018 mpaka 2022
No comments:
Post a Comment