FOLLOWERS

Thursday, November 3, 2011

TANZANIA YAPANDA KIUCHUMI

             Mustapha Mkulo, Waziri wa fedha na uchumi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

               Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tanzania imepanda katika orodha ya nchi zenye uchumi mzuri kutoka katika nafasi ya 187 ambayo imeshikilia kwa muda mrefu mpaka katika nafasi ya 152. hii ni kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa uchumi ya programu ya maendeleo ya umoja wa mataifa ( United Nations Develpoment Program) yenye kichwa cha habari “ Humna Development Report 2011”. Hii ni ripoti ambayo imefanyiwa uchunguzi katika nchi 189 za ulimwengu huu na tanzania kukamata nafasi hiyo ya 152 kati ya nchi hizo 189. maendeleo hayo kiuchumi yamefikiwa huku changamoto zifuatazo zikiwa hazijatolewa utatuzi wa aina yeyote ile na serikali.
1.      kuporomoka kwa kasi ya ajabu kwa thamani ya shilingi ya Tanzania
2.      mgwanyo usio sawa wa mapato ya serikali
3.      mgawanyo usio sawa wa rasilimali za asili
4.      kipato duni cha mwananchi mmoja mmoja
5.      upatikanaji duni wa nishati ya umeme
6.      upatikanaji hafifu wa huduma za afya
7.      kushuka kwa kiwango cha elimu

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...