1. KUTOKANA
NA MHESHIMIWA WAZIRI NA NAIBU WAKE KUWA NJE YA OFISI, KATIBU MKUU WA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AMEPOKEA RISALA YA WAISLAMU NA KWAMBA
ATAIFIKISHA KWA WAZIRI MARA TU ATAKAPORUDI NCHINI.
2. KATIKA
MAZUNGUMZO KUNA MANENO KUWA KUNA WAISLAMU WAMEWEKWA NDANI KUTOKANA NA
ZOEZI LINALOENDELEA LA SENSA. KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI, AMETOA AMRI KWA RPC WOTE KUSITISHA UKAMATAJI WA WATU KUTOKANA
NA ZOEZI LA SENSA NA KWAMBA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAACHIWE KWA
DHAMANA.
3. MAMBO
MENGINE YOTE YALIYOTAJWA KWENYE RISALA YA WAISLAMU YATASHUGHULIKIWA
MARA BAADA YA WAHESHIMIWA MAWAZIRI WENYE DHAMANA HIYO KURUDI NA
MTAJULISHWA.
TAMKO LIMETOLEWA NA,
Signed
MBARAK M. ABDULWAKIL
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
07 Septemba, 2012
Usuli: Leo
tarehe 07 majira ya alasiri, baadhi ya waumini wa madhehebu ya
Kiislamu waliandamana hadi Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi wakiwa na hoja mbalimbali ambazo waliziandika kama Risala kwa
lengo la kuziwasilisha kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Hata
hivyo Waziri na Naibu wake wako safarini hivyo Risala hiyo ilipokelewa
na Katibu Mkuu wa Wizara, Mbarak Abdulwakil, ambaye baada ya
majadiliano alitoa tamko hili hapa juu kwa niaba ya Waziri.
(Imesambazwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
|
No comments:
Post a Comment