Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope (kushoto) akimkabidhi
mchango wa dola 1,000 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel
Ten, Said Kilumbanga kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mchezaji wa
zamani wa timu ya Taifa Stars, Alfonce Modest. Modest kwa nyakati
tofauti aliwahi kuzichezea timu za Simba, Mtibwa Sugar, Pamba, pamoja na
Mlandege ya Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu
Mdau wa Soka na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba
Zakaria Hanspop amekabidhi Fedha Dola za Marekani Elfu Moja kwa Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa "Taifa Stars" Alfonce
Modest ili ziweze kugharimia matibabu ya maradhi ya miguu yanayomkabili
mchezaji huyo kwa sasa.
Zakaria
Hanspope ametoa Fedha Hizo Baada ya Kuelezewa Tatizo linalomkabili
Alfonce Modest na amekabidhi Fedha Hizo Kwa Mratibu wa Matibabu ya
Alfonce Modest Saidi Kilumanga ambaye ni Mtangazaji wa Radio Magic Fm na
Chanel Ten ambaye amekuwa akilishugulikia swala hilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo jijini Dar es salaam Zakaria
Hans Pop amesema ameguswa na matatizo ya mchezaji huyo na kuona ni
muhimu kumsaidia ili aweze kuendelea kupata matibabu
Zakaria
Hans pop ametoa Rai kwa Taasisi, Jamii na watu Mmoja moja wenye
kujiweza kumsaidia Alfonce Modest ili aweze kupata matibabu ya kina
kutokana na maradhi yanayomsumbua.
Taarifa za
Kuumwa kwa Alfonce Modest kwa mara ya kwanza zilitangazwa na Kip[indi
Cha Michezo Cha Radio Magic Fm ambapo Saidi Kilumanga akiongoza kipindi
hicho, aliwaomba mashabiki na wadau wa michezo kwa ujumla kumchangia
mchezaji huyo ili aweze kupata matibabu Hatua ambayo imeanza kupata
mwitikio.
Alfonce Modest ambaye alikuwa akicheza beki ya kushoto katika klabu ya
Simba na Taifa Stars anakabiliwa na maradhi ya Miguu kufa ganzi hali
ambayo imemsababishia maumivu makali na kushindwa kutembea kama kawaida.
Anayeweza Kumsaidia kwa kutoa msaada wa fedha atume kwa njia ya Simu 0718427426 narudia tena 0718427426.
Alfonce
Bado anahitaji Msaada wa Shilingi laki Sita Tu ili kukamilisha mchakato
Huo Ikiwa pamoja na Malazi na Usafiri wa Kurudi kwao Morogoro(KWA HISANI YA LUKAZA BLOG)
|
No comments:
Post a Comment