FOLLOWERS

Sunday, September 2, 2012

HEKAHEKA ZA MOVEMENT FOR CHANGE ZA CHADEMA : MWANDISHI WA CHANNEL TEN DAUDI MWANGOSI AFARIKI DUNIA KATIKA MAPAMBANO YA JESHI LA POLISI NA WAFUASI WA CHADEMA WILAYANI MUFUNDI.


Ndugu zangu,

Jioni ya leo nikiwa katikati ya kufundisha soka ya vijana hapa Iringa nilipigiwa simu na ndugu yangu Allen,  Katibu Wa CHADEMA , Iringa,  akinitaarifu tukio la vurugu zilizotokea Nyololo, Mufindi na hata kifo cha Mwanahabari mwenzetu, mpiganaji  Daud Mwangosi ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari hapa Iringa. Kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa. Inasikitisha sana.  Ni juzi tu nilikutana na kusalimiana nae nje ya ofisi zake kwenye jengo la Mwamoto.

Pole zangu binafsi kwa familia yake ya karibu na mbali.  Tuko nao katika wakati huu mgumu kwao.
Chini hapa ni baadhi ya picha nilizopata kumpiga Daud Mwangosi katika uhai wake.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...