FOLLOWERS

Friday, August 31, 2012

MCHEKI TID AKIWA CHINI YA ULINZI WA POLISI

Imeripotiwa kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa saa nane baada ya kukamatwa kwa kosa la kujaribu kutaka kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba baada ya mahojiano baina ya mama huyo na polisi kwa saa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba. Alipohojiwa na chombo flani cha habari, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, Ni mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe” Alipotafutwa meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari basi wadau wangu mtakua wa kwanza kujua!! ( KUTOKA UJANATZ BLOG)

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...