Nembo ya klabu ya Yanga |
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa kuzingatia majukumu yake
ya kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya
TFF, Ibara ya 49 (1), na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26 (2)
inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi za uongozi kwenye
Klabu ya Yanga:
1.
Wanachama wote wa TFF, ikiwa ni pamoja na Klabu ya Yanga, wanatakiwa kuzingatia
kikamilifu Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF katika kuendesha
shughuli zote za uchaguzi.
2.
Wagombea uongozi wote wa wanachama wa TFF wanapaswa kutimiza masharti ya
uongozi yaliyoanishwa katika Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi.
3.
Kamati za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinapaswa kutimiza kikamilifu majukumu yao ya kulinda Katiba za
wanachama wa TFF na kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF katika
michakato ya uchaguzi.
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga
ilishaelekezwa kufanya hivyo na inakumbushwa kuendelea kuzingatia wajibu huo.
4.
Wagombea uongozi wa wanachama wa TFF wanao wajibu wa kuzifahamu Katiba zao na
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kuomba uongozi kwa kutimiza matakwa
ya Katiba na Kanuni za Uchaguzi.
5.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea maombi ya marejeo (review) dhidi ya uamuzi
wake wa kuwaondoa waombaji uongozi wanne (4) wa Klabu ya Yanga.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inatoa uamuzi ufuatao:
i)
Marejeo yaliyoombwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga yanakiuka Kanuni za Uchaguzi
za Wanachama wa TFF, hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeyakataa.
Kamati inafafanua kuwa hata kama
Kanuni zingekuwa zinaruhusu kufanya marejeo, bado maombi hayo yasingepaswa
kuwasilishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, bali waombaji uongozi
wenyewe.
Pamoja na hayo, sababu za
kuomba marejeo si za msingi kwa kuwa waombaji uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya
Yanga walipewa mwongozo wa kutosha kurekebisha upungufu uliojitokeza katika
mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi za uongozi kwenye Klabu ya Yanga.
ii)
Sara Ramadhani hakutimiza masharti ya kuomba uongozi kwa mujibu wa Ibara ya
10(4) na (5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na kama ilivyoanishwa
kwenye Fomu namba 1 kwa kutojaza fomu na kutoambatanisha vithibitisho vya sifa
za kugombea.
Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuliondoa
jina lake
katika
orodha ya wagombea uenyekikiti wa Klabu ya Yanga.
iii)
Shaaban R. Katwila na Ahmed Waziri Gao wameshindwa kutimiza masharti ya uombaji
uongozi kwa kutowasilisha vyeti halisi kwa ajili ya uhakiki kama
ilivyotakiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya nakala za
vyeti vyao kubainika na NECTA kuwa vina utata.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inaitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutekeleza uamuzi wa kuondoa majina yao kwenye orodha ya
wagombea uongozi wa Yanga.
iv)
Ramadhan Mzimba Kampira ameshindwa kutimiza masharti ya kugombea uongozi kama yalivyo kwenye
Ibara ya 10(5) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF kwa kutoambatanisha
vithibitisho vya sifa za mgombea.
Kwa hiyo, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inasisitiza uamuzi wake na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuondoa jina
lake katika orodha ya wagombea uongozi.
v)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaridhia uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya
Yanga kuwaondoa wafuatao kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi:
(a)
Ally Mayay Tembele
(b)
Abdallah Sharia Ameir
(c)
Jamal Hamisi Kisongo
(d)
Mohamed R Mbaraka
vi)
Wagombea uongozi ambao hawakutajwa hapo juu na ambao walipitishwa na Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga, wametimiza matakwa ya awali ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama
wa TFF na hatua za mwisho za uhakiki wa vyeti vya elimu yao,
zinaendelea.
Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
No comments:
Post a Comment