Askofu anayedaiwa kujiuzulu |
Askofu mpya kabisa kutawazwa imearifiwa kuwa anashikiliwa na mamlaka ya
Uchina baada ya kutangaza kuwa anajiuzulu kutoka Kanisa Katoliki linalokubalika
na Mamlaka ya Uchina.
Thaddeus
Ma Daqin, Askofu wa Shanghai, alitangaza hatua yake ya kujiuzulu kutoka Chama
kijulikanacho kama China
Patriotic Association (CPA) siku ile ambapo alitawazwa wiki iliyopita.Duru za Kanisa Katolika na vyanzo vingine vya kidini vimesema kuwa kiongozi huyo wa dini anashikiliwa ndani ya Seminariyo moja karibu na Shanghai.
Kwa mda mrefu kumekuwepo hali ya kutofahamiana baina ya Uchina na Vatican.
Vatican, iliyomteuwa Askofu Ma, haitambui chama cha CPA kinachokinzana na Kanisa Katoliki na Kanisa Katoliki nchini Uchina halitambui Mamlaka ya Papa.
Waumini wanaokadiriwa kutimu milioni 10 wa huko Uchina wamegawika kati ya wafuasi wa Papa na upande wa pili ukikubaliana na kundi la Chinese Patriotic Catholic Association (CPA).
Taarifa zinasema kuwa Askofu Ma aliuambia ummati wa watu 1,000 kuwa ameamua kujiuzulu ili awezew kushughulikia majukumu yake mapya. Tangazo lake hilo lilifuatiwa na makofi ya waumini , kwa mujibu wa habari za gazeti linalochapishwa huko HongKong la South China Morning Post.
Lakini wadadisi wanasema kuwa hatua hio ilionekana na wakuu wa Uchina kama kejeli na kudharau udhibiti wa Dola la Uchina juu ya viongozi wa Kanisa Katoliki na wengine.
No comments:
Post a Comment