WACHUNGAJI
wanne wa madhehebu ya Kanisa la Pentekoste ambao pia ni Wakurugenzi wa
Taasisi ya Kuendesha na Kusimamia Mchezo wa Upatu (Deci) wamesema
watajitetea kwa njia ya kiapo.
Wiki
iliyopita, washtakiwa hao walipatikana na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma
zinazowakabili za kuendesha na kusimamia mchezo wa upatu kinyume cha
sheria.
Kesi hiyo
ilitajwa majuzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na washtakiwa hao
walisema watajitetea wenyewe kwa njia ya kiapo na kwamba hawatakuwa na
mashahidi wala vielelezo vyovyote.
Baada ya
kusikiliza hoja zote, Hakimu Mkazi Stewart Sanga aliahirisha kesi hiyo
hadi Agosti 20 mwaka huu itakapotajwa tena na kuamuru washtakiwa wapewe
mwenendo wa kesi hiyo.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Dominic Kigendi, Jackson Mtaresi, Timotheo ole Loiting’inye, na Samwel Mtares.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kuendesha na kusimamia mchezo wa kuchangisha fedha kwa
ahadi ya malipo maradufu maarufu kama ‘Panda Mbegu’.
Wanadaiwa
kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2007 na Machi
mwaka 2009 kwenye makao makuu ya Deci yaliyo eneo la Mabibo Mwisho
wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kusimamia mradi wa upatu kwa kuchukua fedha kwa wananchi
kwa ahadi ya kuwapa matumaini ya fedha zaidi kuliko mapato ya mradi
waliokuwa wakiuendesha.
Chanzo; Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment