WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE "TWIGA STARS" |
KAMPUNI ya bima ya
Maxinsure imetoa vifaa vya mazoezi kwa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya
wanawake (Twiga Stars) vyenye thamani ya sh. milioni 1.3. Vifaa hivyo ambavyo
ni jezi, bukta na soksi 20, vizibao (bibs) 20 na mipira miwili vimekabidhiwa
leo (Julai 12 mwaka huu) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amisa Juma.
Akikabidhi vifaa
hivyo, Amisa amesema wamefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa jamii
lakini vilevile wameamua kuiunga mkono timu hiyo ambayo wanajua haina mdhamini
kutokana na vipaji na uwezo ambao umekuwa ukioneshwa na wachezaji wake. Pia amezitaka
kampuni, taasisi, watu binafsi na Serikali kuiunga mkono timu hiyo ili iweze
kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali inayotarajia kushiriki.
No comments:
Post a Comment