Kocha mkuu wa yanga Saintdiet katikati akitangaza kikosi cha kagame mbele ya waandishi wa habari |
ZIKIWA
zimesalia siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Kagame kuanza, Kocha Mkuu wa
Yanga Mbelgiji, Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaocheza
huku akimtema nahodha wake, Shadrack Nsajigwa .
Michuano
hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi, keshokutwa Jumamosi na siku hiyo
itafungua kwa kuanza kucheza na Atletico ya Burundi.
Akitangaza
kikosi hicho, Tom alisema haikuwa kazi rahisi kwake kupata kikosi hicho
kutokana na viwango vya wachezaji wake kwenye tim hiyo.
Saintdiet
alisema, wachezaji ambao amewaacha wasisikitike akiwemo Nsajigwa anatambua
umuhimu kwenye timu na badala yake waendelee na mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mbelgiji
huyo amekitaja kikosi hicho kuwa ni makipa ni Yaw Berko na Ally Mustapha
‘Bartherz’, Mabeki ni Juma Abdul, Godfrey Taita, David Luhende, Oscar Joshua,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani
‘Vidic’, Ladislaus Mbogo.
Viungo
ni Athumani Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Rashidi Gumbo,
Nizar Khalfani, Shamte Ally na Idrisa Rashidi
Washambuliaji
ni Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi na wachezaji aliowaacha ni
Stephene Mwasyika, Ibrahim Job, Said Mohamed, Nsajigwa Omega Seme, Frank Domayo
na Simon Msuva waliopo Timu ya taifa ya vijana ya U-20, Nurdin Bakari mwenye
majeraha ya paja.
No comments:
Post a Comment