FOLLOWERS

Tuesday, June 12, 2012

REDDS MISS WORLD TANZANIA KUFANYIKA JUMAMOSI

Meneja wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya shindano la Redds Miss World Tanzania 2012 litakalofanyika jijini Dar Es Saam katika ukumbi wa 324 Club uliopo Mikocheni,siku ya jumamosi Juni 16,2012.Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International,Hashim Lundenga na Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana kama “Miss World 2012.
Akizungumzia Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012” Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na kumalizika Septemba.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...