FOLLOWERS

Thursday, July 26, 2012

MWENENDO WA HUDUMA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

WAKATI serikali ikiamini Madaktari wamerudi kazini, hali ya matibabu katika Hospital ya Taifa Muhimbili imezidi kudorara. Akizungumza na MTANZANIA katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mmoja wa madaktari (jina tunalo), alisema licha ya madaktari kurudi kazini hali ya matibabu imezidi kupoteza mwelekeo tofauti na hali halisi.
“Huwezi kusema madaktari wamerudi kazini wanatoa huduma…hii siyo kweli, kwa sababu madaktari bado mahitaji yao ya msingi hayajatatuliwa..huwezi kuwa na daktari mwenye manung’uniko kazini, halafu ukasema anatoa huduma bora kwa mgonjwa,
“Mimi nasema ukweli, hospitalini kuna huduma duni zisizokidhi mahitaji ya wagonjwa,nikizungumza kama mwananchi wa kawaida ni kwamba madaktari wanaingia kazini na kusaini lakini hawatoi huduma vizuri,” alisema
“Nawashangaa Watanzania, sijui kwanini wanashindwa kudai haki zao... ukiingia hospitali hazina vifaa lakini utashangaa watanzania wako kimywa,sisi madaktari tukigoma tunaonekana wabaya,” aliongeza daktari huyo.
Akizungumzia hali ya huduma pamoja na nia ya kufanya maandamano, Katibu Mkuu wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Rodrick Kabangila alisema nia ya maandamano ipo palepale.
“Niseme nia yetu ya mgomo ipo palepale, lakini sasa hivi tunashughurikia suala la ‘Intern’s kwani suala hili limeingiliwa na masuala ya kisisa kidogo..kwahiyo ndiyo tunahangaia nao kwanza halafu tutatoa taarifa lini maandamano yetu yanafanyika hivi karibuni,
“Hili suala la Interns, limeingizwa siasa sana kwasababu huwezi kusema unamfutia leseni wakati yeye hana kosa…Serikali ilitaka huyu interns, afanye kazi na nani wakati madaktari ambao ndiyo wanamsimamia yeye walikuwa kwenye mgomo,” alihoji Dk. Kabangila.
Alisema malalamiko yao bado yapo palepale na Baraza la Madakatri Tanganyika haliwatendei haki kwa sababu lipo chini ya Serikali.
“Lile baraza lipo chini ya Serikali, unafikiri haki itatendeka kwetu kweli... sisi tunataka baraza ambalo mwenyekiti wake asiwe mwajiriwa wa Serikali..,” alisema Dk. Kabangila.
Akizungumzia hali ya Dk.Steven Ulimboka, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Edwin Chitage alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
“Dk.Ulimboka anaendelea vizuri kwa sasa na anaendelea kufanya mazoezi ila siwezi kusema atarudi leo wala kesho…hizo taarifa za kwamba atarejea hivi karibuni zitakuwa zimezushwa tu na watu,” alisema Dk. Chitage.
Alitaja baadhi ya hospitali kubwa alizodai kuathiriwa na tukio hilo la kufukuzwa kazi kwa madaktari, kuwa ni Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bugando (Mwanza), KCMC (Moshi) na Hospitali ya Rufaa Dodoma.
Mtanzania

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...