Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha
operesheni yake ya M4C mkoani Iringa na kuitisha kikao cha dharura cha
Kamati Kuu.
Kikao hicho cha Kamati kuu kitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es
Salaam chini ya viongozi wake wakuu Mkiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu
Dr Wilbroad Slaa.
Mkuu wa operesheni M4C Benson Kigaila amesema haiwezekani kuendelea na
operesheni huku polisi wakiua watu kwenye mikutano ya CDM kwa maelekezo
maalum. Amesema Kamati kuu itatoa mwelekeo rasmi wa chama kuhusu hali
hii ambayo haiwezi kuvumiliwa.
Pia inatarajiwa kamati kuu kujadili vitisho vya msajili wa vyama John
Tendwa dhidi ya chama hicho,msajili ambaye watanzania wengi wanaamini ni
kada mwaminifu wa chama tawala.
Source: Tanzania Daima/Majira. |
No comments:
Post a Comment