Makamu
wa Rais - TBF Phares Magesa mwenye fulna nyeupe katikati akizungumza na
kuwaaaga wachezaji hao wengine kutoka kushoto Father Swai Mkurugezi wa
Don Bosco, Kanali Busungu Mkurugenzi wa Michezo JWTZ, Msoffe Katibu Mkuu
TBF, Father Marco don Bosco,na Meja Budodi Mkuu wa Msafara na Kamisha
wa wanawake TBF.
Taarifa kwa Umma
Timu
4 za Tanzania za Kikapu zimeondoka leo kwenda Kampala, Uganda kushiriki
mashindano ya kutafuta bingwa wa kikapu wa kanda ya tano ya Shirikisho
la mpira wa kikapu Duniani - FIBA ( FIBA zone 5 Club Championship).
Timu
zetu zinazoshiri mashindano hayo ni Savio kutoka Don Bosco ambao ndio
Mabingwa wa Tanzania upande wa wanaume na washindi wa pili ABC, na kwa
upande wa wanawake ni Jeshi Stars ambao ndio mabingwa wa Tanzania na
washindi wa pili ni Don Bosco Lioness.
Kila
timu imeondoka na wachezaji 12 na viongozi watatu, mkuu wa msafara ni
Kamishna wa wanawake katika TBF, Meja Specioza Budodi (Mrs.), viongozi
wengine wa juu wa TBF watakwenda Kampala baade akiwemo Ndg. Alexander
Msoffe ambaye ni mjumbe wa bodi ya FIBA kanda ya 5.
Msafara
huo uliagwa rasmi na Makamu wa Rais wa TBF ndg. Phares Magesa katika
viwanja vya ABC - Chang'ombe leo asubuhi, pia walikuwepo Kanali Busungu
ambye ni Mkurugenzi wa Michezo katika JWTZ, Katibu Mkuu wa TBF ndg.
Alexander Msoffe na Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco Father Swai.
Kwa
sasa bingwa kikapu kanda ya 5 ni timu ya Urunani toka Bunjumbura,
Burundi kwa upande wa wanaume na Kenya Ports Authority(KPA) toka Mombasa
, Kenya ambao walichukua ubingwa katika mashindano yaliyofanyika Dar es
Salaam mwaka jana. Mshindano haya yanashikisha timu 2 za wanaume na
wanawake washindi wa juu kutoka katika kila nchi za kanda hii ya 5
inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Ethiopia, Somalia, Sudani, Sudani ya Kusini, Eritrea na Misri.
Pia
mashindano ya kanda ya 5 kwa timu za Taifa mwaka huu yatafanyika Dar Es
Salaam Tanzania mwezi desemba, hivyo ushiriki wa timu zetu 4 katika
mashindano ya vilabu huko Kampala yatasaidia kuwanoa wachezaji wetu na
ni matumani yetu watafanya vizuri na baadae wale watakochaguliwa katika
timu zetu za taifa basi pia watatuwakilisha vizuri.
Tunawashukuru
sana Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Precision Air na wafadhili
wengine walisaidia kufanikisha safari hii na kuwezesha kwa mara ya
kwanza baada ya muda mrefu Tanzania kupeleka nje timu 4 katika
mashindano haya.
Tunaomba
wafadhili wengine waendelee kujitokeza kusaidia michezo na hususani
mchezo wa kikapu ili kufanikisha malengo yetu na kutumiza wajibu wetu
katika jamii yetu.
Tunawatakia kila la heri na tuwaombee Mungu wafanye vizuri katika mashindano haya na kuitangaza vizuri nchi yetu.
Phares Magesa,
Makamu wa Rais- TBF
0784/0767/0713 618320
|
No comments:
Post a Comment