Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina kwa ajili ya
makamishna (match commissioners), watathmini wa waamuzi (referees
assessors) na waamuzi wa daraja la kwanza (class one) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya Ligi Kuu inayotarajia kuanza baadaye mwezi ujao.
Kwa
upande wa makamishna na watathmini wa waamuzi, semina itafanyika jijini
Dar es Salaam kuanzia Agosti 29-30 mwaka huu. Washiriki wanatakiwa
kujigharamia kwa kila kitu; usafiri, malazi na chakula wawapo kwenye
semina.
Semina
kwa waamuzi itafanyika katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza kuanzia
Agosti 31- Septemba 2 mwaka huu. Pia nao watajigharamia kwa kila tu.
Waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni ambao hawakushiriki ile
iliyofanyika Juni mwaka huu na wale walioshiriki lakini hawakufaulu
mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test).
Waamuzi
wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
hawashiriki kwa vile wao wamekukuwa wakishiriki semina zao
zinazoa (KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)
|
No comments:
Post a Comment