FOLLOWERS

Tuesday, August 7, 2012

SOMA HII KUHUSU ZANZIBAR : WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA)

WAZANZIBARI NI JAMII YENYE ASILI NA USTAARABU MSETO (COSMOPOLITAN SOCIETY) NA SIO JAMII YA KIBANTU (KIAFRIKA)

Written by Ahmed Omar Khamis| 04/08/2012


Kabla ya kuja mkoloni wa kiingereza Zanzibar, wazanzibari wa asili mbali mbali kama walivyo hivi sasa walikuwa wakiishi kwa mapenzi makubwa bila ya chuki za ukabila na urangi, au kwa lugha nyengine, waliishi bila ya mimi ni nani na wewe na nani.

Muingereza alikuja kuwaundia wazanzibari vyama vya kikabila na urangi. Vyama hivyo yaani jumuiya za kikabila ni kamavile Arab association, Shirazi association, African association, Indian association na jumuiya nyengine.

Wazanzibari nao wakavishabikia vyama hivi vya kikabila na kila mmoja akawacha kupigania maslahi ya uzanzibari na akapigania maslahi ya kabila lake. Lakini hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa Muengereza, kwani ni sera yake muhimu ya ukoloni ya wagawe uwatawale (divide and rule).


Kuanzia harakati za kutafuta uhuru chama cha ASP na viongozi wake akiwemo kiongozi mkuu Karume waliukejeli na kuupiga vita ukweli kwamba wazanzibari ni watu wa asili na ustaarabu mseto na kujaribu kuyatenga makundi yote ya kizanzibari yalio na asili zake kutoka nje ya bara la Afrika kama vile waarabu, wahindi, magoa nk. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata washirazi wenye asili zao kutokeaIranambao ndio wanaofanya asilimia kubwa ya wazanzibari nao walipigwa vita.

Kama hilo halitoshi hata wakomoro wenye ngozi nyeupe lakini wenye asili zao kutokea katika bara la Afrika nao walikejeliwa na kukataliwa. Kwa viongozi wa ASP mzanzibari namba moja au mzanzibari asilia na mwenye hadhi kubwa ni lazima awe mwafrika mwenye ngozi nyeusi. ASP iliupigia kelele, kuunadi na kuutukuza uafrika pamoja na ngozi nyeusi na kuzidharau jamii zote za kizanzibari zilizobaki.

Kabla ya mapinduzi ASP na viongozi wake walijaribu kuwaheshimu washirazi wakifahamu bila ya wao na wingi wao ushindi kwa ASP ingelikuwa ndoto. Mara tu baada ya mapinduzi na ASP kushika hatamu chuki dhidi ya ushirazi na washirazi zikadhihirika.

Serikali ya Karume ilipambwa na viongozi wenye asili zao kutokea bara hususanTanganyika. Hii inajionyesha hata kwa majemedari wa mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzo lilikuwa na watu wengi zaidi wenye asili zao kutokea bara. Hii iliwafanya wafikirie kwamba serikali ya mapinduzi ni ya wazanzibari wa asili za bara na waliobaki ni watu wa daraja la pili. Baada ya mapinduzi Karume aliwataka watu wote wenye asili ya kikomoro kuomba uzanzibari (Burgess 2009:204). Kwa kuwa Karume mwenyewe alikuwa na asili yake kutokeaMalawialiwaogopasanawas hirazi. Katika akili yake Karume aliwaona washirazi ni watu wanaoringa na kujidaikamawazanzibari halisi. Hivyo basi aliwalazimisha washirazi nao kubadilisha makabilayao.

Washirazi wengi walilikataa agizohilola Karume hususan wapemba. Wengi wa washiraziPembawalisema wao hawana kabila jengine mbadala mpaka Karume atakapowapatia baba wengine. Hivyo basi hali halisi ya ugozi na ukabila ilipamba moto zaidi baada ya mapinduzi kuliko kabla.

Wapigaji na wachezaji wa ngoma hiyo chafu ya ukabila baada ya mapinduzi walikuwa viongozi wa serikali ya mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzokamavile Karume mwenyewe, Seif Bakari na Abdalla Said Natepe, Mungu awarehemu.


Baada ya mapinduzi vitabu vyote vya historia vilivyofundisha ukweli kuhusuZanzibar, maisha ya masultani, na urithi wa ustaarabu mseto vilichomwa moto (Burgess 2009). Tukio moja la uchomaji huo lilifanyika eneo la Lumumba Unguja mbele ya macho ya maelfu ya watu. Badala yake mwenyekiti wa Youth league, Seif Bakari aliandika kitabu kipya kilichokua kikisomeshewa watoto mashuleni. Katika kitabu chake hicho, Seif Bakari anadai kuwa yote yaliopita kabla ya mapinduzi yalikuwa si chochote bali ni dhiki na dhuluma.

Katika kuzidi kuchonga chuki miongoni mwa wazanzibari weusi dhidi ya wenye ngozi nyeupe, Abdalla Said Natepe ambae ni mjumbe wa mwanzo wa baraza la mapinduzi na mjumbe wa kamati ya watu 14 alikuwa akifanya mikutano ya hadhara kuwaaambia watu hadithi za uzushi. Miongoni mwa hadiuthi hizo ni kuwa waarabu waliwalazimisha waafrika kupanda minazi kisha wakawa wanajifundishia shabaha kwa kuwatungua kwa risasi.

Hadithi nyingine ni kuwa waarabu waliwalazimisha wanawake wa kiafrika kufyagia barabara kwa maziwayaona waja wazito wa kiafrika walip[asuliwa ili bibi wa kiarabu ajue mtoto amekaaje tumboni. Mafundisho haya yamekuwa yakitolewa mashuleni kwa muda mrefu ili kutia sumu katika akili za watoto wakishirazi na kifrika dhidi ya waarabu.


Nyimbo za uafrika dhidi ya asili nyengine zote ziliendelea kuimbwa ndani serikali ya mapinduzi kupitia warithi wake wenye misimamo mikali ya uhafidhina wa ugozi na umapinduzi kwa lengo la kulinda malengo na uhalali wa mapinduzi hayo.

Kuthibitisha kasi na nguvu za uhafidhina huu na chuki dhidi ya watu wasiokuwa na asili ya kiafrika ndani ya Zanzibarni maneno ya Omar Ramadhani Mapuri, ambae yeye mwenyewe ana asili yake kutoka Tanzaniabara, aliyekuwa Waziri wa elimu na Naibu waziri kiongozi katika awamu ya nne ya Rais Salmin Amour. Kupitia kitabu chake, Zanzibar Revolution, Achievements and Prospects, kitabu ambacho kinazungumzia kiwango cha juu cha ukabila katika enzi za ustaarabu duniani, Mapuri ameweka wazi hisia zake kali dhidi ya watu wasiokua waafrika ndani yaZanzibar.

Lengo kuu la Mapuri katika kitabu chake ni kuwataka wazanzibari wenye asili za kiafrika kuungana dhidi ya kile anachokiita chokochoko na uchokozi wa nchi za magharibi na waarabu ambao chini kwa chini kwa mujibu wa Mapuri wanataka kurudisha tena ushawishi waoZanzibarkama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Umoja huu ambao Mapuri anawaasa wazanzibari ndio ule ule uliotumika katika harakati za uhuru na mapinduizi ya 1964.


Katika kitabu chake pia Mapuri anakana kwa nguvu zote mauwaji yaliyofanywa na mapinduzi ya 1964 na kwa mujibu wa mawazo yake yale yanayoripotiwa kuwa ni upotezaji wa roho za watu kwa mgongo wa mapinduzi ya 1964 ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba watu waliokufa kutokana na mapinduzi hayo ni wachache mno. Hata hivyo katika kitabu chake anadai kuwepo kwa nyaraka zinazobainisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani iliyopinduliwa ya kutaka kuuwa raia wengi wa kiafrikakamani kulipiza kisasi kwa mauwaji ya waarabu waliouliwa kufuatia uchaguzi wa juni 1961 ijapokuwa hakubainisha katika kitabu chake nyaraka hizo zilipo.

Mapuri anadai nyaraka hizo zinathibitisha kwamba serikali ilipanga kuuwa waafrika sitini (60) kwa kila mwarabu mmoja aliyeuliwa Juni 1961. Mapuri pia anadai nyaraka hizo zinathitisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani kuzitaifishamalizote za waafrika wasio na asili za kizanzibari. Hakumalizia hapo Mapuri pia ameandika kwamba Serikali ya Shamte ilikuwa na lengo la kuwafanya watumwa wazanzibari wote wenye asili ya kiafrika na hatimae Zanzibar kutangazwa kama ardhi ya waarabu.

Kikubwa zaidi ambacho pia Mapuri amewatanabahisha wazanzibari katika kitabu chake ni azma ya Serikali ya Shamte iliyopinduliwa kuwauwa watoto wote wa asili ya kiafrika na wanawake wenye asili ya kiafrika kulazimishwa kuolewa na waarabu kwa malengo ya kutokomeza ngozi nyeusiZanzibar.

Alichokifanya Mapuri bila shaka lilikuwa si jambo geni katika historia yaZanzibar. Ni marudio tu ya yale yalioanzia miaka ya 1960 ya mapambano ya makabila katika kugombania kumezwa, kufunikwa au kutokomezwa na makabila mengine.


Ni jambo la kushangaza mno kwa enzi ambayo vuguvugu la kihistoria la ukabila na uasili tayari limeshasahaulika, kiongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaranapika upya migawanyiko ya wazanzibari kwa misingi ya rangi, ngozi na wanakotokea mababu zao.

Kiongozi kama huyu bila shaka ana dhima kubwa ya kuwaunganisha wazanzibari walio na asili na utamaduni wa kila namna karibu kutoka pembe zote za dunia lakini badala yake anashajihisha na kuhimiza umoja na muungano wa baadhi ya wazanzibari dhidi ya wenzao. Hata hivyo sio Mapuri peke yake katika viongozi wa leo wanaopiga kelele za ukabila na uasili ndani ya Zanzibarya kisasa.

Wapo wenzake Mapuri ambao wao wamefika mbali zaidi kwa kudai kwamba vijukuu na vinying’inya vya waarabu hawapaswi kupewa madaraka ya Zanzibarkwa kunasibika kwao na kabila la wapinga mapinduzi ya 1964. Katika kitabu chake, Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru, Harith Ghassany analizungumzia hivi suala hili.


“Fikra ya uzalendo ya Pan-Africanism ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa na misingi kwamba kila asiye “Muafrika” ni mgeni (wakuja) Afrika na kwa maana hiyo pia ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu na mipana ndani ya Zanzibar.

Kinyume chake kila aliyekuwa ana asili ya Kiafrika (kibantu) na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu ndani ya Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuweza kutawala kwa sababu tu ni “Muafrika.” Hapa sharti ifahamike kwanza kuwa neno “Afrika” linatokana na neno Ifriqiya, ambayo wanahistoria wanathibitisha ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Tunisia.

Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociologist) aliyeishi miaka 676 nyuma, amemzungumza katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus Bin Qays Bin Sayfi. Kwa mujibu wa Ibn Khaldum Mfalme huyu aliishi wakati wa Nabii Musa au labda kidogo kabla yake. Ibn Khaldum anathibitisha kuwepo kwa mfalme huyo kutoka Yemen ambaye jina lake hilo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina “Afrika”.

Mawazo yaliyoenezwa kila upande ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa dahari nyingi. Mawazo haya yanatokana na fikra kuwa “Bara la Waafrika” ni Bara la watu weusi tu. Watu weusi hao tena ni wale wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu hao bila shaka wawe hawana kabisa asili au uhusiano wowote na Waarabu.

Wenye mawazo haya bila shaka walisahau kuwa wanalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Kaskazani katika nchi za Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea na Mauritius. Halkadhalika mawazo hayo yamewatenga wazungu wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Kenya. Pia mawazo hayo yamewatenga Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya watu ambayo yana chimbuko lake katika bara hili” (Gassany 2010).


Wazanzibari ni watu walio na asili zao nyingi na ustaarabu mchanganyiko ulizoanzia mbali. Asili za kiarabu, ki-pashia, kihindi, kitanganyika, kiganda, kikenya, kimsumbiji, kikomoro, kinyasa, kisumeri, kiassiri, kisomali, kiabisini, kifoniki, kidiba, kidebule, kireno, kibaluchi, kikurdi, kijojia, kichina, kisrilanka nk Wengi wao ni machotara, hakuna awezae kukaza mdomo akamtukana mbantu, akija akitanabahi kumbe kamtukana babu yake, au akakaza mdomo akamtukana mwarabu, akitanabahi kamtukana mama yake.

Uarabu, ubantu, uhindi, na asili nyengine zote za wazanzibari zilizopo kamwe hazibandukani na uzanzibari na bila ya kundi moja tu katika hayo ni sawa na mwanadamu asivyokamilika akikosa baadhi ya viungo vyake.


Tunaishukuru sana serikali ya ya Dr Shein ya Umoja wa kitaifa kwani imefanikiwa kufuta madoadoa ya kibaguzi baina ya wazanzibari wenyewe kwa wenyewe na kuusimika ule ustaarabu mseto (cosmopolitanism) unaomtambua kila mzanzibari kua ni mzanzibari bila ya kuangalia rangi yake, nywele zake pua yake.

Wazanzibari tusurudi nyuma haya ya kufunzwa kubaguana ndio yaliyotufikisha hapa na kuipoteza nchi yetu na hatimae kuingia mikononi mwa Tanganyika. Tuungane kwa umoja wetu turudishe heshma ya Zanzibar yetu yenye mamlaka kamili kama ilivyowahi kutamalaki hapo kabla ya 1964.


Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
..KUTOKA JAMII FORUMS 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...