MWENYEKITI MPYA WA KLABU YA YANGA YA JIJINI DAR YUSUPH MANJI AKIONGEA NA WACHEZAJI LEO ASUBUHI ALIPOWATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KLABU HIYO MITAA YA TWIGA |
UONGOZI mpya wa klabu ya Yanga leo asubuhi ulitembelea makao makuu ya
klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kukutana na
kuzungumza na wachezaji.
Viongozi hao wapya waliokuwepo kwenye msafara huo ni mwenyekiti, Yussuf Manji, makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Bin Kleb, Mussa Katabalo na George Manyama.
Katika msafara huo, pia walikuwemo wajumbe wa kamati ya utendaji katika uongozi uliopita, Salum Rupia na Mohamed Bhinda.
Katika kikao chake hicho na wachezaji, Manji aliwataka wawe na imani kubwa kwa uongozi mpya kwa vile wamejipanga vyema kuhakikisha timu inapata huduma zote muhimu na kwa wakati na pia inapata ushindi katika kila mechi watakazocheza.
Manji aliwaeleza wachezaji hao kuwa, wanapaswa kucheza kwa ari na kujituma kwa vile matatizo yaliyojitokeza msimu uliopita hayatakuwa na nafasi katika uongozi wake.
Katika kikao hicho, wachezaji wa Yanga walionekana kuwa na furaha kubwa huku kila wakati wakipiga makofi ya kumshangilia mfadhili huyo wa zamani wa klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment