FOLLOWERS

Tuesday, July 17, 2012

WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPEWA SEMINA

Mwezeshaji na mkufunzi  wa mafunzo ya habari za biashara na uchumi Bw. Mnaku Mbani akitoa maelezo juu ya uandishi wa habari za Biashara na Uchumi, mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza.

baadhi ya washiriki waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkufunzi wa semina hiyo

waandihi wa habari wapatao 19 waliojitokeza katika semina hiyo inayotarajiwa kuendelea mpaka siku ya alhamisi na imeanza siku ya jumatatu

Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuifanya jamii kupata uelewa zaidi kuhusu masuala mwelekeo wa taifa.
Akitoa elimu hiyo, muwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Mnaku Mbani amesema lengo la semina hiyo ni kuwanoa wanahabari nchini kuwa na uelewa katika masuala ya uchumi.
Mbani amesema hatua hiyo imekuja kutokana na waandishi wengi kutojikita katika uandishi huo wa habari za biashara na uchumi na hivyo eneo hilo kutotendewa haki licha ya kuwa muhimu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...