wachezaji wa timu ya taifa kwa ajili ya mashindano ya olimpiki wakionyesha bendera walipokuwa wakiondoka uwanja wa ndege wa mwalimu Juilius Nyerere leo |
hapawakielekea kupanda ndege tayari kwa safari yao |
TIMU ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya
Olimpiki imeondoka leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere kwenda London, Uingereza, huku ikiwa na matumaini ya kurudi na medali.
Timu hiyo ya Tanzania yenye
wanamichezo sita ambao ni wa Kuogelea, Ngumi za Riadhaa na Riadha imeondoka
jana majira ya jioni kushiriki michuano hiyo inayoanza Julai 27 hadi Agosti 12
mwaka huu, yakishirikisha nchi 205.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege, mmoja
wa wachezaji hao, bondia wa ngumi za ridhaa, Seleman Kidunda, amejinasibu
kufanya maandalizi ya kutosha kumuwezesha kurudi na medali, ingawa pia aliomba
dua za Watanzania. “Naenda
kulipigania taifa kuhamasisha mabondia ambao wanadhani kuwa Tanzania
haiwezi. Lengo ni kuitangaza nchi na Afrika, hasa ukizingatia kuwa haya ni
mashindano makubwa duniani. Muhimu kwa Watanzania kutuombea dua,” alisema
Kidunda.
No comments:
Post a Comment