FOLLOWERS

Wednesday, July 11, 2012

MISS UTALII KAGERA KUFANYIKA JUMAMOSI


Shindano la kumsaka Miss Utalii mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika ukumbi wa Linas Club mjini Bukoba, siku ya tarehe 14-7-2012 kuanzia saa, mbili usiku.

Katika shindano hilo jumla ya Warembo 15 watapanda jukwaani kuchuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera, ambapo watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu, kitalii, kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni, urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.  

Pia shindano hilo litasindikizwa na burudani mbalimbali za Ngoma za asili, muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Diamond Musica na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Agcox Burchaman kutoka Uganda, Maua na BK Sunday. 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...