Bondia Ramadhani Shauli akiwa ameushika Mkanda wa I.B.F Africa wakati
ulipokuwa ukioneshwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar
es salaam ukitokea USA mkanda huo utakaogombaniwa na Shauli na
bondia Sande Kizito kutoka Uganda utafanyika siku ya Iddi pili katika
ukumbi wa Diamond Jubilee kushoto ni
Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Madaraka Nyerere na Promota wa mpambano
huoMkurugenzi wa Kitwe General Traders, Lucas Rutainirwa Mtanzania
Ramdhani Shauri atapanda ulingoni siku ya Idd pili kupambana na bondia
Sande Kizito kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Africa
katika uzito wa unyoja (Featherweight).
Shauri anayefanya mazoezi
yake Ubungo, maeneo ya Mabibo na anafundishwa na kocha mzazi anayetamba
kuwa na mabondia wenye nidhamu na vipaji vya hali ya juu.
Ramdhani
Shauri ni bondia chipukizi mwenye umri wa miaka 19 na historia yake ya
ngumi inafurahisha kila anayeisoma na kuisikia. Ana haiba nzuri
inayovutia na anafananishwa na bondia Sugar Ray Leonard wa Marekani
kutokana na haiba yake na upiganaji wake.
Sugar Ray Leonard
alitamba katika miaka ya 70 na 80. Shauri ni Mfalme anayekuja na hivi
sasa anatishia maisha ya mabondia wengi katika bara la Afrika.
Ramadhani
Shauri ana nidhamu ya hali ya juu na maisha yake katika ngumi
yanafurahisha kwa jinsi anavyoishi kwa nidhamu na kufanya mazoezi ya
kujijenga katika ngumi. Katika maisha yake anajiepusha sana na matatizo
ambayo vijana wengi wametumbukia kama vile uvutaji wa bangi, ngono zembe
na mambo mengine yasiyo na malengo katika maisha.
Huyu ndiye
kweli Mfalme anayekuja katika ngumi za kulipwa na nchi yetu imepata
bahati kubwa sana kuwa na kipaji cha bondia kama huyu.
Mpambano wa Shauri umepewa jina la “The Rumble in the City of Heaven’s Peace” (Vurumai katika Jiji la Amani).
Watanzania, tumuezi mwenzetu Ramadhani Shauri anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment