Mkuu wa mkoa wa Tanga Bi Chiku Galawa |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku
Galawa, amepiga marufuku shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu katika
wilaya ya Handeni na kuunda tume ya kuchunguza uharibifu wa mazingira
unaotokana na vitendo vya ukataji wa miti ya mbao na mkaa.
Mkuu huyo wa mkoa amechukua
uwamuzi huo baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa wa misitu ambapo aliwakamata
watu wawili kwa uhalibifu hao uliokuwa ukifanyika kwa kisingizio cha kuanzisha
mashama mapya.
Bi. Galawa amesema kuwa tume hiyo
itawashirikisha watumishi wa Idara ya Maliasi na miisitu, Jeshi la Polisi
pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya handeni.
No comments:
Post a Comment