FOLLOWERS

Wednesday, July 18, 2012

MHESHIMIWA MNYIKA AMALIZA KUHOJIWA

MHESHIMIWA JOHN JOHN MNYIKA MBUNGE WA UBUNGO - CHADEMA           Mrejesho wa Mwisho/Update: Nimemaliza kutoa maelezo ya kurasa 12 pamoja na mambo mengine nimesema wazi kuwa kabla ya mkutano nilipewa taarifa kuwa kuna kikundi cha vijana wa CCM kimepangwa kuvuruga mkutano, hata baada ya kuwaambia Polisi wahakikishe ulinzi, Polisi waliwaachia vijana hao warushe mawe wakati Bwana Waitara akihutubia.

Taarifa za mauaji tulizipata usiku baada ya kurejea Singida Mjin
i na zilitolewa na RPC.

Hivyo sifahamu uhusiano wowote uliopo kati ya mauaji na mkutano wa CHADEMA uliomalizika kwa amani. Na nimewaambia sikutoa lugha yoyote ya matusi wala uchochezi bali nilieneza sera na wananchi wakataka turudi tena na tukawaahidi kuwa tulikwenda kwenye maandalizi ya Operesheni Sangara ya Singida nzima!

Nimewaambia, tuna ushahidi wa video na tutautoa mahakamani.

John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA),
18 Julai, 2012

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...