WILLIAM MHANDO, MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ALIYESIMAMISHWA KAZI |
Uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando unatokana na bifu linalosemekana kuwapo kati ya Mhando na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; lakini katibu mkuu huyo ametumia udhaifu wa serikali na tanesco kumwadhibu Mhando.
Inasemekana sababu inayotolewa na Katibu Mkuu ni kwamba Mhando alimdharau kwa kutompa taarifa kabla ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme wa hivi karibuni. Kwa mantiki hiyo, akamlima Mhando barua akisema anahujumu shirika. Hata hivyo, wananchi na watumishi wa Tanesco wanajua kuwa anayehujumu Tanesco ni serikali, ambayo inalinyima shirika hilo pesa ilizoahidi kwa ajili ya miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, na kulizuia shirika hilo kuuza umeme kwa faida, kwa sababu za kisiasa.
Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.
source east africa radio breaking news
No comments:
Post a Comment