FOLLOWERS

Sunday, July 15, 2012

DK SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM ZANZIBAR

Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt.Amani Abeid Karume,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dkt. Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, kwa pamoja wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo  katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,wakiwa  katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kilipofanyika kikao hicho leo.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...