Tanzania imeanzisha mradi mkubwa wa
kuzalisha gesi nchini ambao unaweza kuubadili uchumi wa nchi katika njia za
msingi, viongozi walisema.
Mtambo wa Kuzalishia umeme wa
Ubungo unatumia gesi kuzalishia umeme. Pamoja na kuhifadhi umeme unaosafirishwa
kuelekea bara, Tanzania itaweza kuongeza uzalishaji wa umeme wa kutosha pamoja
na kuuza nje ya nchi, viongozi wamesema. [Deodatus Balile/Sabahi]
Tanzania imesaini mkataba na kampuni tatu za
China tarehe 21 Julai ambazo zitaanza ujenzi hivi karibuni wa bomba la kilometa
512 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, haya yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi.
Maswi aliiambia Sabahi mradi huo utagharimu
shilingi trilioni 1.86 (Dola za Marekani bilioni1.2), zilizotolewa
kwa mkopo kutoka Export-Import Benki ya China. Ujenzi unatarajiwa
kukamilika ndani ya miezi 18, alisema.
Mpango unahusisha ujenzi wa bomba la inchi
36 kwa umbali wa kilomita 487 na bomba la inchi 24 kwa umbali wa kilomita 24,
likiunganisha bara hadi kwenye chanzo cha gesi iliyoko Somanga Fungu, kisiwa
kidogo katika Bahari ya Hindi, alisema Maswi.
Maswi alisema gesi inayotumika kuzalisha
umeme kwa sasa inagharimu Dola za Marekeni 0.42 (shilingi 663) kwa megawati.
"Lakini kwa kuwa na bomba hili
tunashindwa kuamini," alisema. "Gharama za gesi hiyo hiyo, inayotosha
kuzalisha yuniti moja, itashuka hadi Dola za Marekani 0.02, karibia shilingi
32, baada ya kukamilika kwa ujenzi. Hii itachangia kiasi kikubwa kwa Uchumi wa Tanzania."
Tangu mwaka 2006, Tanzania imekumbwa na muda
wa kupimia watu umeme, ambao Maswi alisema ana matumaini litatuliwa mradi huu
utakapokamilika na uzaalishaji kuanza.
Shirika la Maendeleo ya Teknolojia ya
Petroli China, Shirika la Uhandisi wa Bomba la Petroli na Shirika la Uhandisi
wa Bomba la Petroli la China
yamepewa mkataba wa kujenga bomba hilo.
Yona Killagane, mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), alisema bomba hilo jipya litakuwa na
uwezo wa kusafirisha futi 784 mchemraba za gesi kwa siku, ambazo zitazalisha
megawati 3920 za umeme.
Mahitaji ya sasa ya Tanzania ni
megawati 720 kwa siku. Kwa hiyo, kwa kuzalisha megawati 3,920 kupitia hifadhi
ya gesi ya ndani, nchi itakuwa na ziada ya megawati zaidi ya 3,000 za kutumiwa
kwa ajili ya kusafirisha nje au kuanzisha viwanda vipya, Maswi alisema.
Mwanauchumi Benson Mahenya, mkurugenzi wa
Andrew's Consulting Group (ACG), anasema mradi huo una uwezekano wa kuinua
uchumi.
"Ni dhahiri, gesi ni chanzo rahisi
zaidi cha umeme na inafaa zaidi," aliiambia Sabahi. "Kama punguzo
litamfikia mtumiaji wa mwisho, Watanzania watapata nafuu."
Mahenya alisema bei ndogo ya gesi
itahamasisha uwekezaji mpya katika viwanda mbalimbali kupitia kupunguzwa kwa
gharama za uzalishaji. "Matokeo ya ongezeko yatakuwa ya kipekee. Kwa
gharama za umeme kupungua, tutakuwa na viwanda vingi ambavyo vitazalisha fursa
nyingi za kazi." alisema.
Hata hivyo, alieleza kuwa na shaka kuhusu ni
kwa muda gani soko litaona manufaa yanawafikia watumiaji wa mwisho. Alisema kwa
kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lina madeni makubwa, faida
inayotarajiwa haitaonekana kwa angalau miaka miwili baada ya ujenzi kukamilika.
"Watatumia faida hiyo kubwa kulipia
deni na kununua mitambo mipya," Mahenya alisema. "Huenda ifikapo
2025, tutakapofanya uchaguzi ujao, gesi itatumika kama
silaha ya kisiasa kupitia upunguzaji wa bei kwa uniti moja ili kuwaonesha
wapiga kura serikali iliyo madarakani inawajibika ipasavyo."
Ofisa Mwandamizi wa Utafiti na Maendeleo wa
TPDC Charles Sangweni alisema hifadhi ya gesi ya Tanzania itadumu kwa zaidi ya
miaka 100, Daily News la Tanzania
liliripoti. Akiba ya gesi iliyopatikana Songosongo, Mnazi Bay, Mtwara, Noria,
Mikindani na Mkuranga katika eneo ya Pwani inafikia ujazo wa futi mchemraba
trilioni 30.
Alisema akiba ya gesi iliyopo ina thamani ya
shilingi trilioni 626 (Dola bilioni 397) na Tanzania inaweza kufanya mtaji
katika maliasili kwa kuwasambazia majirani zake.
No comments:
Post a Comment