FOLLOWERS

Wednesday, November 6, 2013

WIZI WA PIKIPIKI WASABABISHA MAUAJI MBEYA


KUTOKA MBEYA YETU BLOG :MTU mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi.

Wananchi hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana majira ya saa mbili asubuhi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga, alisema kuwa  marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki  eneo la Utengule.

Alisema, baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa kumtia nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita moja.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...