Chadema
jana ilifanya Mkutano wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa
hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.
Mkutano
huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo
vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali
alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya
kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa
CCM tangu mwaka 1983.
Katika
kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee
Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali
alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee
kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi
wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.
Katika
mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA
wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya
mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa
shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee
Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.
Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.
Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.
Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi
KWA HISANI YA LUKAZA BLOG
|
No comments:
Post a Comment