na mwandishi wetu
MIKAKATI
na kampeni za majitaka zenye lengo la kumchafua Mbunge wa Jimbo la
Busega mkoani Simiyu, Dk. Titus Kamani, zimeanza kubainika kwa
kumhusisha na tena na tuhuma za mauaji.
Dk. Kamani, ambaye ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitosa kuwania nafasi ya
Mwenyekiti
wa Mkoa mpya wa Simiyu, ameanza kuchafuliwa akihusishwa na tuhuma za
kutaka kumuua aliyekuwa mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, aliwahi
kueleza bayana kuwa wamefanya uchunguzi wa kina na kubaini Dk. Kamani
hahusiki na tuhuma hizo na kwamba, waliotuhumiwa wameshafikishwa
mahakamani.
“Hatumtafuti Dk Kamani,
tukimhitaji tutampata lakini katika uchunguzi wetu tumebaini tuhuma
hizo hazimuhusu," alikaririwa Kamanda Barlow baada ya kuibuka kwa uvumi
kuwa mbunge huyo alikuwa akisakwa na polisi.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, jana, Dk. Kamani
amesema kumekuwepo na kampeni chafu za kuhakikisha jina lake linachafuka
ili kudhoofisha harakati zake za kukitumikia Chama.
Amesema kuwa tangu
alipojitosa kuwania nafasi hiyo, kumekuwepo na mikakati ya kumchafua
inayofanywa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo waliopo ndani ya CCM na
kwamba, hilo amelibaini na atalifikisha kwenye vikao husika.
Dk. Kamani katika taarifa yake amesema kuwa, mbinu chafu hizo zimekuwa zikisukwa na wanasiasa hao kwa lengo la kumchafua na kumchonganisha na wapigakura wake pamoja na jamii imuone kuwa hafai.
“Makovu
na visasi vya kushindwa katika uchaguzi uliopita kamwe havitaiharibu
Busega wala kunidhoofisha kuwatumia wananchi wangu.
Nafahamu hizi ni mbinu
chafu kwa ajili ya kuniharibia katika harakati zangu za kuwania nafasi
ndani ya Chama," alisema katika taarifa hiyo.
Tayari watu wanaotuhumiwa kuhusika katika njama za kutaka kumuua Dk. Chegeniwameshapandishwa kizimbani kujibu mashitaka hayo.
(KUTOKA : SUFIANI MAFOTO)
|
No comments:
Post a Comment