Sensa ni muhimu kwa nchi yoyote kwa maana kwamba ni sherti serikali ijue idadi ya watu wake na mahali wanapoishi.
Takwimu na taarifa hizo ndio msingi wa upangaji wa mipango yoyote ya
huduma na maendeleo. Kwa akili yangu finyu, huu ni ukweli usiopingika.
Kama kuna sehemu ambapo watu hawajahesabiwa, sehemu hiyo itaonekana iko
wazi; haina watu. Kwa maana hiyo, hakutakuwa na msingi wowote wa
kuiingiza sehemu hiyo katika mpango wa huduma au maendeleo.
Sehemu itakayoonekana haina watu itawekwa kando katika mipango hiyo ya
huduma na maendeleo. Sasa basi, endapo kulikuwa na watu sehemu hiyo,
ambao walisusia sensa, wasije wakajitokeza baadaye na kulalamika kuwa
wanaonewa.
|
No comments:
Post a Comment