Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi, akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga
Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dkt. Alphoncina Mbinda, wakati wa hafla
maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa
hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya
wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni
baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu
Wilaya ya Kinondoni, Stanley
Mkandawile, (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu
Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.
|
No comments:
Post a Comment