FOLLOWERS

Tuesday, July 24, 2012

TSH 210 MILIONI ZATENGWA KWA AJILI YA KITUO CHA AFYA IGAWILO

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya imetenga Sh210 milioni ambazo zitatumika kukamilisha wodi ya watoto na wajawazito, ununuzi wa majokofu vikiwamo vifaa kwa ajili ya upasuaji ili kukiwezesha Kituo cha Afya Igawilo kuanza kufanya kazi kama hospitali ya wilaya.

Hayo yalisemwa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Hilda Ngoye aliyetaka kujua ni lini kituo hicho kitaanza kufanya kazi kama hospitali ya wilaya.

Amesema taarifa ya ukaguzi huo ilipendekeza kwamba kituo hicho kipandishwe hadhi na kuwa hospitali ya jiji.

Amesema halmashauri imeomba kuajiri watumishi 14 wa kada za afya kwa ajili ya kituo hicho. Majaliwa alisema kimsingi wizara kupitia kamati iliyokagua kituo hicho iliridhia baadhi ya huduma zikiwamo huduma za mama na mtoto na upasuaji dharura kwa kina mama ziendelee kutolewa katika kituo hicho zikiwa na hadhi ya hospitali ya wilaya.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...