BAADHI YA VIONGOZI WALIOKUWA NA JUKUMU LA KUZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO WAKIWA WAMEKETI JUKWAA KUU |
BAADHI YA UMATI WA WANANCHI WALIOJITOKEZA KUHUDHURIA MKUTANO HUO JANA |
WAKEREKETWA WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WAKIONYESHA ISHARA YA CHAMA, NYUMA NI MWENDESHA BAISKELI AKIWA NA BANGO KAMA LINVYOONEKANA |
ALLY BANAGA ALIYEHAMIA CHADEMA KUTOKA CCM AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeendelea na operesheni yake ya
M4C kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kujua mizizi ya matatizo
mbalimbali yanayowakabili watanzania nchini kote, na kukiweka chama
karibu zaidi na wananchi.
Safari hii ilikuwa ni zamu ya wakazi
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kutembelewa na makamanda wa chama
hicho hapo jana wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho Mh
Godbless Lema.
Mh Lema aliambatana na viongozi na makamanda
wengine wakiwemo wanachama wapya waliohamia chama hicho hivi karibuni
kutokea CCM. Miongoni mwao ni pamoja na James Ole Millya, Ally Bananga
na Alphonce Mawazo.
Jumla ya mikutano saba ilifanyika kwa siku ya
jana, sita ikifanyika kwa kuruzu maeneo tofauti ya Simanjiro kwa
kutumia helcopta na baadae kumalizia na mkutano mkubwa wa jioni katika
uwanja wa shule ya msingi Mirerani iliyopo eneo la Mirerani. Lema,
Mawazo na Millya ndio waliotumia chopa na wengine walitumia gari mpya za
chama hicho kwa njia za barabara kutokea Arusha Mjini
No comments:
Post a Comment