Mtanzania Adam Nditi katika moja ya hekaheka uwanjani dhidi ya timu ya vijana ya manchester united |
Adam Nditi |
Mchezaji wa Tanzania Adam Nditi jana amesaini mkataba
‘rasmi’ kama mchezaji wa kulipwa wa klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza.
Kupitia Twitter jana ameandika;
“Leo ni siku muhimu na ya kukumbuka kwangu na familia yangu na
ningependa kumshukuru Mungu kwa kila kitu nilichonacho na vile navyokuwa.”
“Kuna wakati nakumbuka nilichoka
kimwili na kiakili lakini baada masaa kadhaa ya mazoezi , kujituma na kufanya kazi
kwa biddi naweza kusema hatimaye ndoto yangu imetimia.”
“I'd like to say well done to
@Anditi3 for signing his pro contract with chelsea today! Official chelsea player! Well done bro! #cfc”
alipongezwa na miongoni mwa wachezaji aliokuwa nao Chelsea Academy
aitwaye Dom Solanke.
”My bro @Anditi3 signed his
professional contract with Chelsea
FC, well done man.” aliandika mwingine.
"Thanks again everyone for
saying all the good luck and only God knows what's ahead waiting for me,"
Nditi alitweet.
Adam alijiunga na Chelsea Academy mwaka 2008.
Alicheza kwa mara ya kwanza
msimu wa 2010-11 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa
timu ya vijana ya Chelsea iliyoshinda kombe la FA mwaka 2011-12 na
mara zote alikuwa akiingia kipindi cha kwanza isipokuwa kwenye mechi ya fainali
dhidi ya Blackburn Rovers, ambapo aliingia kipindi cha
pili.
Adam Nditi alizaliwa tarehe
18 September 1994 mjini Zanzibar.
Hongera sana Adam.
No comments:
Post a Comment